2017
Manabii Watuongoze
September 2017


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Septemba 2017

Manabii Watuongoze

Miaka michache iliyopita, nilikuwa nimeketi katika chumba cha Hekalu la Salt Lake ambapo Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili hukutana mara moja kwa wiki. Nilitazama juu kwenye ukuta ulio mkabala na Urais wa Kwanza, na pale niliona picha ya kila mmoja wa Marais wa Kanisa.

Huku nikizitizama, watangulizi wangu—kuanzia Nabii Joseph Smith (1805–1844) kufikia Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008)—Nilifikiria, “Nina shukrani kwa mwongozo ya kila mmoja wao.”

Hawa ni wanaume wakuu ambao kamwe hawakuyumbayumba, kamwe hawakusita, na kamwe hawakushindwa. Hawa ni watu wa Mungu. Ninapofikiria kuhusu manabii wa siku zetu ambao nimewajua na kuwapenda, ninakumbuka maisha yao, tabia zao, na mafundisho yao yenye mwongozo.

Rais Heber J. Grant (1856–1945) alikuwa Rais wa Kanisa wakati nilipozaliwa. Ninapotafakari kuhusu maisha yake na mafundisho yake, ninaamini tabia ambayo Rais Grant alionyesha kwa mfano zaidi ni kushikilia—kushikilia vile vitu ambavyo ni vizuri na venye uadilifu.

Rais George Albert Smith (1870–1951) alikuwa Rais wa Kanisa wakati nilihudumu kama askofu wa kata yangu katika Jiji la Salt Lake. Alitambua ya kwamba kuna vuta nikuvute kubwa inayoendelea kati ya Bwana na adui. “Ikiwa utabaki katika upande wa Bwana wa laini,” alifundisha, “Utakuwa chini ya ushawishi wake na hutakuwa na hamu ya kutenda maovu.”1

Niilitwa kuhudumu kama Mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili mwaka wa 1963 na Rais David O. McKay (1873–1970). Alifundisha kuzingatia wengine kupitia jinsi alivyoishi maisha yake. “Ukristo wa Kweli,” alisema, “ni upendo kupitia vitendo.”2

Rais Joseph Fielding Smith (1876–1972), mmojawapo wa waandishi wakuu wa Kanisa, alikuwa na kanuni elekezi katika maisha yake ikiwa ni usomi wa kiinjili. Alisoma maandiko bila ya kukoma na alikuwa ufahamu wa mafunzo na mafundisho yanayopatikana katika kurasa zake kama mtu yeyote nimewahi kumfahamu.

Rais Harold B. Lee (1899–1973) alihudumu kama rais wangu wa kigingi nilipokuwa mvulana. Dondoo aliyoipenda zaidi ilikuwa “Simameni katika mahali pa takatifu na wala msiondoshwe.”3 Aliwahimiza Watakatifu wawe na uelewa wa, na kusikiliza, ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Ninaamini ya kwamba kanuni elekezi katika maisha ya Rais Spencer W. Kimball (1895–1985) itakuwa ni kujitolea. Alikuwa kamili, dhahiri amejitolea kwa Bwana. Alikuwa pia amejitolea kuishi injili.

Wakati Rais Ezra Taft Benson (1899–1994) alipokuwa Rais wa Kanisa, aliniita nihudumu kama Mshauri wake wa Pili katika Urais wa Kwanza. Upendo ulikuwa kanuni yake elekezi, iliyopo katika dondoo yake aliyoipenda zaidi, iliyosemwa na Mwokozi: “Mnapaswa kuwa watu wa aina gani? Amini, nawaambia, hata vile nilivyo.”4

Rais Howard W. Hunter (1907–95) alikuwa mwenye kutafuta wema daima katika wengine. Daima alikuwa mkarimu; daima alikuwa mnyenyekevu. Ilikuwa ni heshima kwangu kuhudumu kama Mshauri wake wa Pili.

Rais Gordon B. Hinckley alitufundisha kutenda bora zaidi. Alitoa ushuhuda wa nguvu juu ya Mwokozi na huduma Yake. Alitufundisha kwa upendo. Kuhudumu kama Mshauri wake wa Kwanza ilikuwa ni heshima na baraka kwangu.

Mwokozi hutuma manabii kwa sababu Anatupenda. Wakati wa mkutano mkuu Oktoba hii, Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka wa Kanisa tena watakuwa na nafasi ya kushiriki neno Lake. Tunatekeleza jukumu hili kwa umakini na unyenyekevu mkubwa.

Tumebarikiwa kiasi gani kwamba Kanisa lililorejeshwa la Yesu Kristo lipo duniani na limejengwa juu ya mwamba wa ufunuo. Ufunuo unaoendelea ndicho kiini cha injili ya Yesu Kristo.

Na tujiandae kupokea ufunuo binafsi unaokuja kwa wingi wakati wa mkutano mkuu. Na mioyo yetu ijazwe na uamuzi wa kina wakati tunapoinua mikono yetu kuwakubali manabii na mitume walio hai. Na tuweze kuelimishwa, tuinuliwe, tufarijiwe, na tuimarishwe wakati tunaposikiliza jumbe zao. Na tuwe tayari kujitolea upya kwa Bwana Yesu Kristo—Injili Yake na kazi Yake—na kuishi kwa azimio jipya katika kutii amri Zake na kutenda mapenzi Yake.

Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: George Albert Smith (2011), 191.

  2. Teachings of Presidents of the Church: David O. McKay (2003), 181.

  3. Mafundisho na Maagano 87:8.

  4. 3 Nefi 27:27.

Chapisha