2018
Wasiliana Naye Kila Wakati, Kila Mahali, Kila Njia
January 2018


Kanuni za Ualimu wa Kutembelea, Januari 2018

Wasiliana Naye Kila Wakati, Kila Mahali, Kila Njia

Ualimu wa Kutembelea unahusu kuhudumia. Yesu alihudumu wakati wowote na kila mahali. Tunaweza kufanya vivyo hivyo.

“Kuhudumia” ni kutoa huduma, kutunza, na msaada ambao unachangia faraja au furaha ya mtu mwingine. Ualimu wa kutembelea unahusu kugundua njia za kuwahudhumia wale tunaowatembea. Yesu Kristo aliwahudumia wote—wakati wowote na mahali popote. Yeye alilisha watu elfu tano, akamfariji Mariamu na Matha wakati wa kifo cha kaka yao, na alimfundisha mwanamke kisimani injili Yake. Alifanya hivyo kwa sababu ya upendo Wake wa kweli.

Kufuatia mfano Wake, kama walimu watembeleaji tunaweza kumjua na kumpenda kila dada tunayemtembelea, tukikumbuka kwamba upendo ndiyo msingi wa yote tunayofanya. Tunaposali kwa ajili mwongozo wa kujua jinsi ya kumhudumia yeye na kumsaidia kuimarisha imani yake, ‘malaika hawawezi kuzuiliwa kutoka kwa hawa wenzi wetu.”1

Kutoka kuanzishwa kwa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama katika mwaka wa 1842 hadi leo, uhudumiaji wa wanawake umebariki wengi. Kwa mfano, Joan Johnson, mjane wa miaka 82, na mwenzi wa ualimu wa kutembelea wanafundisha jirani ambaye ana miaka 89, na ana homa ya mapafu. Wao waliona kwamba jirani yao hakuwahitaji tu mara moja kwa mwezi, kwa hivyo walianza kumjulia hali kila wiki ana kwa ana au kwa simu.

Kwa walimu wengine wa kutembelea, kutuma ujumbe mfupi au barua pepe ili kutia moyo inaweza kuwa kitu bora cha kumfanyia dada mwezi huo. Kufanya miunganiko binafsi na kusikiliza kwa mtazamo wa upendo ni kiini cha ualimu wa kutembelea. Tekinolojia ya kisasa na mazungumzo ya ana kwa ana yanayoenziwa hutusaidia kufanya hivyo wakati wowote, kila mahali, na katika njia nyingi.2 Hio ndiyo kuhudumia jinsi Yesu alivyofanya.

Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 454.

  2. Ona Handbook 2: Administering the Church (2010), 9.5.1.

Chapisha