Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Januari 2018
Kipawa cha Toba
“Ni jukumu letu kuinuka kutoka uhafifu hadi ukamilifu, kutokana na ushinde hadi kufaulu.” Rais Thomas S. Monson alifundisha. Wajibu wetu ni kuwa bora zaidi wenyewe. “Moja ya zawadi kubwa ya Mungu kwetu ni furaha ya kujaribu tena, kwani hakuna kushindwa kamwe kunakopaswa kuwa mwisho.”1
Tunahusisha kila mara mwanzo wa mwaka mpya na maazimio na malengo. Tunaazimia kuboreka, kubadilika, kujaribu tena. Labda njia muhimu zaidi tunayoweza kujaribu tena ni kushikilia kile Rais Monson anachokiita “kipawa cha toba.”2
Katika dondoo kutoka katika mafundisho yake tangu awe Rais wa Kanisa, Rais Monson ametushauri “tutumie damu ya upatanisho wa Kristo kwamba tupokee msamaha wa dhambi zetu, na mioyo yetu isafishwe.”3
Muujiza wa Msamaha
“Sisi wote tumeshafanya chaguzi zisizo sahihi. Ikiwa tayari hatujarekebisha chaguzi kama hizo, nawahakikishia kwamba kuna njia ya kufanya hivyo. Mchakato huu unaitwa toba. Mimi nawasihi mrekebishe makosa yenu. Mwokozi wetu alikufa kukupa wewe na mimi ile zawadi ya heri. Ingawa njia si rahisi, ahadi ni halisi: ‘Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji’ [Isaya 1:18]. ‘Na Mimi, Bwana, Sitakumbuka wao tena’ [M&M 58:42]. Usiweke maisha yako ya milele hatarini. Ikiwa umetenda dhambi, mapema unavyoanza safari yako ya kurudi, ndivyo utapata imani tamu na furaha ambayo uja kwa muujiza wa msamaha.”4
Rudi kwenye Njia
“Ingawa ni lazima tuchague kwa busara, kuna wakati ambapo tutafanya uchaguzi usio wa busara. Zawadi ya kutubu, iliyotolewa na Mwokozi wetu, inatuwezesha kurekebisha mwelekeo wetu, ili tuweze kurudi katika njia ambayo itatuongoza hadi kwenye ule utukufu wa selestia tunaoutafuta.”5
Njia ya Kurudi
“Ikiwa mmoja wenu amejikwaa safarini mwake, nampa matumaini kwamba kuna njia ya kurekebisha. Njia inaitwa toba. Ingawa njia ni ngumu, wokovu wako wa milele unaitegemea. Ni kipi kinachoweza kuwa cha kustahili zaidi jitihadi zako? Ninawasihi mfanye uamuzi papa hapa na mchukue hatua zinazohitajika kutubu kikamilifu. Mapema unavyofanya hivyo, ndivyo haraka itakavyowezekana kwako kuhisi amani na utulivu na matumaini yaliyozungumziwa na Isaya [ona Isaya 1:18].”6
Watu Wanaweza Kubadilika
“Tunahitaji kukumbuka kwamba watu wanaweza kubadilika. Wanaweza kuweka nyuma yao mazoea mabaya. Wanaweza kutubu dhambi. Wanaweza kuhimili ukuhani kwa ustahiki. Na wanaweza kumtumikia Bwana kwa bidii.”7
Kuwa Msafi Tena
“Kukiwa na uwezekano wa makosa yoyote katika maisha yako, kuna upenyo wa kuokoka. Komesha uovu wowote. Zungumza na askofu wako. Shida yoyote, inaweza kutatuliwa kupitia toba inayofaa. Unaweza kuwa msafi mara ingine tena.”8
Nafasi Muhimu ya Mwokozi
“Muhimu katika mpango huu ni Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Bila dhabihu Yake ya upatanisho, yote yangepotea. Haitoshi, hata hivyo, kuamini tu katika Yeye na utumishi Wake. Tunahitaji kufanya kazi na kujifunza, kutafuta na kusali, kutubu na kuboreka. Tunahitaji kujua sheria za Mungu na kuziishi. Tunahitaji kupokea ibada Zake za kuokoa. Ni kwa kufanya hivyo tutapata furaha ya milele.”9
© 2018 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/17. Idhini ya kutafsiri: 6/17. Tafsiri ya First Presidency Message, January 2018. Swahili. 15045 743