2021
Kwa Kusudi Hili Nalizaliwa
Desemba 2021


UJUMBE WA URAIS WA ENEO

Kwa Kusudi Hili Nalizaliwa

Kadiri nilivyotafakari mambo tuliyofanya ili kuimarisha kumbukumbu nzuri za familia juu ya Krismasi, uzingativu wa utimilifu wa fursa ambayo kuzaliwa kwa Kristo kumeniletea, umeniamsha kwenye hamu kubwa ya kufanya zaidi.

Katika matukio kadhaa wakati wa huduma yake duniani, Kristo aliona inafaa kufafanua sababu ya yeye kuwepo duniani.

Punde tu baada ya Shetani kumuacha kufuatia jaribio lisilo na mafanikio la kumjaribu Yeye na kuvuruga kusudi Lake, Yesu alikwenda kwenye sinagogi huko Nazareti. Alisimama na akichagua andiko ambalo lilitimiza lengo Lake kutoka katika kitabu cha Isaya, Yeye alitangaza kwa mkusanyiko:

“Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema, amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa . . .

“Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu” (Luka 4:18–19, 21).

Katika tukio lingine, akiwajibu wanafunzi Wake kuhusiana na kutojali Kwake kwenye vilio vya mwanamke Mkananayo akitafuta huruma Yake juu ya bintiye aliyepagawa na pepo, alifundisha: “Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (ona Mathayo 15:24).

Alitumia kipindi hiki kilichohitimishwa na uponyaji wa binti wa mwanamke ili kujulisha lengo la huduma Yake ya duniani na kutambua nani walikuwa hadhira Yake iliyokusudiwa. Nyumba ya Israeli haikuwa tu wale waliokuwa wa familia hiyo kutokana na nasaba. Ilikuwa pamoja na wale wote waliojumuishwa kwa imani Kwake, kama vile mwanamke Mkananayo alivyoonesha. Na bado katika tukio jingine Yeye alitenga muda kumuelimisha Nikodemo kuhusu lengo la maisha Yake duniani:

“Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa:

“Ili kila mtu aaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele katika yeye.

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

“Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

“Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

“Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

“Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.

“Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu” (ona Yohana 3:14–21).

Katika siku zake za mwisho duniani, kama ambavyo alijibu swali la Pontio Pilato ikiwa alikuwa Mfalme wa Wayahudi, Yeye kwa mara nyingine alitangaza tena lengo la kuzaliwa Kwake:

“Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu: kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi: lakini ufalme wangu sio wa hapa.

“Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu” ona (Yohana 18:36–37).

Kusherehekea ujio wa Yesu Kristo duniani kupitia uzoefu wa kuzaliwa ambao sote tunaushiriki pamoja Naye, lakini kwa upande Wake kwa muujiza ulio sambamba na hilo wa bikira kushika mimba, unapaswa kutufanya sisi kutoa umakini maalum kwenye umuhimu wa maisha Yake ya duniani kwetu sisi binafsi. Maandiko hapo juu yanatualika sisi kila mmoja kujichunguza:

Ni kwa njia zipi tuko katika hitaji la uponyaji ambao kuzaliwa kwa Kristo kuliwezesha hilo kwetu na kwamba tunaweza kuufikia wakati wowote kupitia msimamo wa imani isiyoyumba Kwake?

Ni kwa njia zipi tunajumuisha katika shughuli zetu, onyesho la imani Kwake ambalo linatustahilisha kuwa wa nyumba ya Israeli kama vile alivyofanya mwanamke Mkananayo?

Tunapozingatia maamuzi ambayo tumefanya na matendo ambayo tumetenda mwaka huu, je tunaweza kusema kwa ujasiri kwamba daima tumeenenda katika ukweli na kwamba kama matokeo, tumebarikiwa kwa nuru zaidi na hekima zaidi? Na kama si hivyo, je tuko radhi kuweka msimamo wa kufanya hivyo kuanzia sasa na kuendelea?

Ni jinsi gani tunaweza kuendelea kuisikia sauti Yake?

Ni matarajio yangu kwamba maswali haya yanatusaidia kuichukulia Krismasi si tu kama tukio ambalo tunaliwekea alama wakati wa mwezi wa mwisho wa mwaka na kisha kujikita kwenye shughuli zingine wakati tukingojea Desemba inayofuata ije tena. Krismasi inapaswa kutusaidia kuweka akiba na kufanya mapitio ya vile sisi tulivyo hasa kama wafuasi wa Kristo. Tunapaswa kutumia fursa hii kutafuta kuelewa vizuri zaidi kile tunachoweza kutenda zaidi ili kufanya kuzaliwa Kwake kuwe na matokeo makubwa na baraka nyingi katika maisha yetu sisi binafsi na familia.

Miaka mingi, familia yetu hufanya juhudi kusherehekea Krismasi pamoja. Kati ya Desemba 25 na 31 ya kila mwaka, tunachagua siku ambapo tunakusanyika mahala pamoja na kufurahia muda na kila mmoja. Tunapeana habari mpya juu ya mambo mazuri ya kile kilichotokea kwenye kila familia kwa kipindi cha mwaka. Kadiri watoto zaidi walivyozaliwa na kukua, tumejumuisha shughuli za kuburudisha ambazo zimeongeza kwenye hisia za furaha za kila tukio. Japokuwa sote tunajichukulia kama wafuasi wa Kristo, kwa sababu ya tofauti katika imani na shughuli za kidini, kwa kawaida kila familia inakuwa na huduma ya Krismasi nyumbani kabla ya kuja kwenye kusanyiko kubwa la kifamilia. Shughuli za hivi karibuni na endelevu ni kwamba wakati mwingine mtu huleta zawadi hususan kwa watoto, kitu ambacho kinaongezea kwenye matarajio yao ya tukio. Hizi ni nyakati nzuri.

Kadiri nilivyotafakari mambo mazuri ambayo tumefanya kuimarisha kumbukumbu hizo nzuri za familia za Krismasi, uzingativu wa utimilifu wa fursa ambayo kuzaliwa kwa Kristo kumeniletea, umeniamsha kwenye hamu kubwa ya kumsaidia kila mtu kufanya zaidi.

Ndiyo, kila mshiriki wa familia yetu anahitaji zaidi nguvu ya uponyaji ya Mwokozi. Na tunaweza kila mmoja kufanya zaidi ili kustahili kama washiriki wa nyumba ya Israeli. Sote tunahitaji kutembea zaidi kwa uimara katika ukweli na hekima inayotolewa na injili ya Yesu Kristo, hata wakati tunapojitahidi kuisikiliza sauti Yake mara nyingi zaidi. Hivyo, natumia fursa ya kukumbuka Krismasi mwaka huu kufanya zaidi ili kufokasi kusanyiko la familia yetu kubwa kwenye jinsi tunavyoweza kila mmoja kufanya hili.

Ninawaalika mfanye vivyo hivyo. Katika jina la Yesu Kristo, Amina.

Joseph W. Sitati aliidhinishwa kama Sabini Mkuu Mwenye Mamlaka mnamo April 2009. Amemuoa Gladys Nangoni; wao ni wazazi wa watoto watano.