2021
Uwakilishi kutoka Sudan Watembelea Maeneo ya Kanisa ya Salt Lake
Desemba 2021


YA MTANDAONI PEKEE

Uwakilishi kutoka Sudan Watembelea Maeneo ya Kanisa ya Salt Lake

“Hisia yetu kuhusu [Utah] ni kwamba ni jamii ambayo imetufunza jinsi inavyoweza kuzishinda changamoto . . . Hisia yetu nyingine ni jinsi kanisa hili linavyoweza kufanya kazi sambamba na jamii yake kuimarisha kanuni za kibinadamu.” Naserldeen Mofarih, Waziri wa Rasilimali na Maswala ya Dini wa Sudan, hivi karibuni alitoa maneno haya katika matembezi aliyoyafanya huko makao makuu ya Kanisa Jijini Salt Lake, Utah. Bwana Mofarih alisindikizwa na uwakilishi wa viongozi wa serikali kutoka Sudan. Kwa pamoja, walikutana na viongozi waandamizi wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Wakati wa matembezi, uwakilishi wa watu sita kutoka Sudan walitembelea Maeneo ya Hekalu, Maeneo ya Ustawi wa Kanisa, Kituo cha Msaada wa Kibinadamu na Ghala Kuu la Askofu. Pia walikutana na Urais wa Kwanza wa Kanisa, Urais wa Eneo la Afrika ya Kati Kaskazini Mashariki na washiriki wa urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi. Kwa kuongezea, walitembelea msikiti ulioko Bonde la Salt Lake. Ili kuona picha na kusoma zaidi kuhusu tukio hili, tembelea ukurasa wetu wa Facebook wa Afrika ya Kati: https://www.facebook.com/churchofjesuschristafricacentral/