“Ibrahimu na Sara,” Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Februari 2022
“Ibrahimu na Sara”
Ujumbe wa kila mwezi wa gazeti la Rafiki, Februari 2022
Ibrahimu na Sara
Vielelezo na Apryl Stott
Ibrahimu alikuwa nabii. Mungu alifanya agano na Ibrahimu pamoja na mkewe, Sara.
Mungu aliahidi kuwabariki. Aliwaambia watakuwa na watoto. Ibrahimu na Sara waliahidi kumfuata Mungu.
Ibrahimu na Sara walitunza ahadi yao. Lakini hawakuwa na watoto kwa muda mrefu. Walizidi kuwa wazee sana.
Hatimaye, Ibrahimu alipokuwa na umri wa miaka 100 na Sara akiwa na miaka 90, walipata mtoto wa kiume. Walimwita Isaka. Walijua Mungu alikuwa amewabariki.
Ninaweza kumwamini Mungu. Wakati mwingine baraka haziji papo hapo. Lakini Mungu daima hutimiza ahadi zake.
Ukurasa wa Kupaka Rangi
Ninaweza kumwamini Mungu
Bonyeza kwenye picha ili kupakua.
Kielelezo na Apryl Stott
Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni amekusaidia ulipokuwa unaogopa au mwenye huzuni?
© 2022 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly Friend Message, February 2022. Swahili. 18313 743