2022
Sakramenti: Njia ya Kumkumbuka Mwokozi
Aprili 2022


“Sakramenti: Njia ya Kumkumbuka Mwokozi,” Liahona, Aprili 2022.

Ujumbe wa kila mwezi wa Liahona, Aprili 2022

Sakramenti: Njia ya Kumkumbuka Mwokozi

Picha
placeholder altText

Chakula cha Mwisho, na Simon Dewey

Usiku huo kabla hajasulubishwa, Yesu Kristo alikutana na Mitume Wake kwenye Chakula cha Mwisho. Aliwapa sakramenti kwa mara ya kwanza. Alieleza kwamba ilikuwa njia ya wao kumkumbuka. Sakramenti ni ibada ambapo tunakula mkate na kunywa maji ili kukumbuka Upatanisho wa Kristo. Mkate huashiria mwili wa Kristo, na maji huashiria damu Yake.

Tunaipokea sakramenti kila Jumapili wakati wa mkutano wa sakramenti. Tunaimba wimbo huku wenye ukuhani wakimega mkate vipande vidogo vidogo.

Wenye Ukuhani walioumega mkate wanasema sala maalum. Sala hizi zinapatikana katika Mafundisho ya Dini na Maagano 20:77, 79. Sala zinatukumbusha kile ambacho tumemwahidi Baba wa Mbinguni na kile ambacho ametuahidi.

Wenye ukuhani wengine wanapitisha sakramenti kwa waumini wa kata au wa tawi. Tunapopokea sakramenti, tunamkumbuka Mwokozi na dhabihuYake kwa ajili yetu. Pia tunaahidi kuyashika maagano (ahadi) tuliyofanya na Baba wa Mbinguni.

Picha
msichana akipokea mkate wakati wa mkutano wa sakramenti

Tunakuwa na staha wakati sakramenti inabarikiwa na kupitishwa. Ni wakati wetu kufikiria kuhusu maisha, mafundisho na Upatanisho wa Yesu Kristo. Pia tunaweza kufikiria jinsi tunavyoweza kuiga mfano Wake.

Chapisha