2022
Kupokea Endaumenti Yako
Oktoba 2022


Dondoo za Kitabu cha Maelezo

Kupokea Endaumenti Yako

Je, umewahi kusikia viongozi wa ukuhani au waumini wa Kanisa wakikuhimiza “kujitayarisha kupokea endaumenti”? Yaweza kuwa unajiuliza hicho ni nini. Kitabu cha Maelezo ya Jumla kinafafanua.

“Neno endaumenti humaanisha ‘zawadi’”, kinasema Kitabu cha Maelezo ya Jumla. “Endaumenti ya hekaluni kiuhalisia ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo kwayo Yeye huwabariki watoto Wake. Endaumenti inaweza kupokelewa ndani ya mahekalu matakatifu pekee. Baadhi ya zawadi ambazo waumini hupokea kupitia endaumenti ya hekaluni ni pamoja na:

  • “Ufahamu mkubwa wa malengo na mafundisho ya Bwana.

  • “Nguvu ya kufanya yote ambayo Baba wa Mbinguni anataka watoto Wake wafanye.

  • “Mwongozo wa kiungu wakati wakimtumikia Bwana, familia zao pamoja na wengine.

  • “Ongezeko la tumaini, faraja na amani.”

Unapokaribia kumbukizi ya mwaka mmoja ya ubatizo wako, Kitabu cha Maelezo ya Jumla kinapendekeza kufanya mambo yafuatayo ili kujitayarisha kwa ajili ya endaumenti yako.

Kwanza, anza kuhudhuria madarasa ya maandalizi ya kwenda hekaluni.

Pili, panga kufanya mahojiano na askofu ili kupokea kibali cha hekaluni.

Tatu, panga tarehe na hekalu ili kupokea endaumenti yako.

Ni uzoefu mpya na wa kuvutia wa kupokea endaumenti yako. Unaweza kuwa na maswali kabla ya kwenda na pengine maswali zaidi baada ya kwenda. Ni mchakato wa kujifunza hata kwa watu ambao wamekwenda mara nyingi. Uelewa wako utaongezeka pale unapoendelea kurejea hekaluni.

Muhtasari

  1. Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

  2. Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha