2022
Kwa Nini Tunalipa Zaka
Disemba 2022


“Kwa Nini Tunalipa Zaka,” Liahona, Dis. 2022.

Ujumbe wa kila mwezi wa Liahona, Disemba 2022

Kwa Nini Tunalipa Zaka

Picha
sarafu zikiwa pamoja

Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho hutoa moja ya kumi ya kipato chao Kanisani. Hiyo huitwa zaka. Fedha hutumika kwa ajili ya kazi ya Kanisa ulimwenguni kote.

Zaka ni nini?

Moja kati ya amri za Mungu ni kulipa zaka, ambayo ni moja ya kumi ya kipato chetu, kwenda kwenye Kanisa Lake. Wakati tunapolipa zaka, tunaonyesha shukrani zetu kwa Mungu kwa baraka tulizonazo. Tunaonyesha kwamba tunamwamini Bwana na kwamba tuko tayari kumtii katika yote.

Picha
Watu wakileta vitu kwa Melkizedeki kama matoleo ya zaka

Melkizedeki—Mweka Hazina, na Clark Kelley Price

Mafundisho ya Agano la Kale

Watu wa Mungu wamelipa zaka tangu wakati wa Agano la Kale. Kwa mfano, Abraham alilipa zaka (ona Mwanzo 14:18–20). Sheria ya zaka pia ilifundishwa na manabii wa kale, ikijumuisha Musa na Malaki (ona Mambo ya walawi 27:30–34; Nehemia 10:35–37; Malaki 3:10).

Urejesho wa Sheria ya Zaka

Mnamo mwaka 1838, Nabii Joseph Smith alimuuliza Bwana namna ambavyo waumini wa Kanisa wangetakiwa kulipa zaka. Jibu la Bwana limeandikwa kwenye Mafundisho na Maagano 119, ambayo inasema kwamba waumini wa Kanisa wanatakiwa kutoa moja ya kumi ya ongezeko kwenda Kanisani (ona mstari wa 4). Viongozi wa Kanisa wamefundisha kwamba “ongezeko” humaanisha kipato.

Picha
Watu wakishikana mikono wakati mmoja akitoa bahasha kwa mwingine.

Picha na Jamie Dale Johnson

Jinsi ya Kulipa Zaka

Tunaweza kulipa zaka kwa kujaza fomu kwenye mtandao kupitia donations.ChurchofJesusChrist.org. Au tunaweza kujaza fomu ya karatasi na kumpa fedha mshiriki wa uaskofu au urais wa tawi. Fedha yote hutumwa makao makuu ya Kanisa, ambapo viongozi wa Kanisa (Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi) kupitia sala huamua jinsi itakavyotumika.

Baraka

Bwana ameahidi kwamba wale wanaolipa zaka watabarikiwa kimwili na kiroho. Zaka pia huwabariki watoto wote wa Mungu kwa fursa za kujifunza kuhusu Yeye na kukua katika injili.

Picha
Hekalu la Salt Lake

Jinzi Zaka Inavyotumika

Fedha ya zaka inatumika katika kujenga Kanisa la Bwana kote ulimwenguni. Hii hujumuisha kujenga mahekalu na majengo mengine ya Kanisa, kuchapisha maandiko matakatifu na makala zingine, kudhamini shule inayomilikiwa na Kanisa na kusaidia katika kazi ya historia ya familia na ya kimisionari.

Tamko Juu ya Zaka

Mara moja kwa mwaka, waumini wa Kanisa wanakutana na askofu (au rais wa tawi) kumwambia kama ni walipa zaka kamili.

Zaka Hulipia Nini

Picha
Hekalu la Oakland California

Picha ya Hekalu la Oakland California na Longin Lonczyna Jr.

Picha
nakala za Kitabu cha Mormoni katika lugha tofauti
Picha
nyumba ya ibada

Chapisha