Liahona
Kuamini katika Kristo kabla Yeye Hajaja Tena
Aprili 2024


“Kuamini katika Kristo kabla Yeye Hajaja Tena,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Apr. 2024.

Ujumbe wa kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana , Aprili 2024

Yaromu

Kuamini katika Kristo kabla Yeye Hajaja Tena

Wanefi walikuwa na imani kabla Mwokozi hajaja, na sisi tunaweza kuwa na imani kabla Yeye hajaja tena.

Yesu Kristo anawatembelea Wanefi.

Je, umewahi kufikiria ingekuwaje kuamini katika Mwokozi kabla ya Yeye kuja duniani? Wanefi wa kale ilibidi wafanye hivyo tu—“walimtazamia Masiya, na kuamini katika yeye kuja kana kwamba tayari amekwisha kuja” (Yaromu 1:11).

Siku hizi, tunayo kumbukumbu ya kimaandiko na kihistoria ambayo inashuhudia kwamba Yesu Kristo aliishi, alikufa, na amefufuka tena. Tunaamini katika Kristo ambaye tayari alikwisha kuja. Lakini pia tunaamini katika Mwokozi ambaye atakuja tena.

Kabla ya Kristo Kuja, Wanefi Walikuwa na Imani ya:

Mfalme Benyamini na mke wake wakisali

Kusamehewa dhambi zao

“Yeyote atakayeamini kwamba Kristo atakuja, hao watapokea msamaha wa dhambi, na kushangilia kwa shangwe kuu zaidi, kama vile tayari amekuja miongoni mwao” (Mosia 3:13; msisitizo umeongezwa).

Enoshi

Wanajisamehe wenyewe.

“Na sauti ikanijia, ikisema: Enoshi, umesamehewa dhambi zako. … Kwa hiyo, hatia yangu ikafagiliwa mbali. Na nikasema: Bwana, je, inafanywa vipi? Na akaniambia: Kwa sababu ya imani yako katika Kristo, ambaye wewe kamwe hujamwona wala kumsikia. Na miaka mingi itapita kabla yeye hajajidhihirisha katika mwili; … imani yako imekufanya mkamilifu.”(Enoshi 1-5-8; msisitizo umeongezwa).

Yakobo akihubiri

Kufanya miujiza.

“Tulijua kuhusu Kristo, na tulikuwa na matumaini ya utukufu wake maelfu mengi ya miaka kabla ya kuja kwake. … Kiasi kwamba tunaweza kweli kuamuru katika jina la Yesu na hata miti inatutii sisi, au milima, au mawimbi ya bahari” (Yakobo 4:4, 6; msisitizo umeongozwa).

Moroni akiandika kwenye mabamba

Pokea ufunuo.

“Kulikuwa na wengi ambao imani ilikuwa imara kupita kiasi, hata kabla Kristo hajaja, ambao hawangeweza kuzuiliwa kutoka ndani ya pazia, bali kweli waaliona kwa macho yao” (Etheri 12:19; msisitizo umeongezwa).

Kabla Yesu Kristo Hajaja Tena, Sisi Tunaweza Kuwa na Imani Ya:

Kusamehewa, kujisamehe wenyewe, kufanya miujiza, na kupokea ufunuo (kama Wanefi).

mvulana akiimba kanisani

Tunajiandaa wenyewe kwa ajili ya ujio Wake.

Tunapojitahidi kushika maagano yetu, tunajitayarisha kuishi katika ufalme wa selestia. “Kwani tazama, maisha haya ndiyo wakati wa watu kujitayarisha kukutana na Mungu; ndiyo, tazama, wakati wa maisha haya ndiyo siku ya watu kufanya kazi yao”(Alma 34:32).

vijana mbele ya hekalu

Kuutayarisha ulimwengu kwa ajili ya ujio Wake.

Tumealikwa na Rais Russell M. Nelson kuwa sehemu ya “ile kazi kuu duniani”—ya kukusanya Israeli. “Baba Yetu wa Mbinguni amehifadhi wengi wa roho zake wazuri—labda, naweza kusema, timu Yake bora zaidi—kwa ajili ya awamu hii ya mwisho. Roho hao wazuri—wachezaji hao bora, hao mashujaa—ni ninyi!”1

wasichana wakikumbatiana

Kuwa na matumaini wakati wa nyakati ngumu.

Mwokozi atakapokuja tena, wenye haki wataishi katika amani. Mwokozi atatawala, na yasiyohaki yatafanywa sawa. “Kwa kuwa Bwana atakuwa katikati yao, na utukufu wake utakuwa juu yao, naye atakuwa mfalme wao na mtoa sheria wao” (Mafundisho na Maagano 45:59).

msichana

Kutumaini katika Ufufuko.

Wanadamu wote watafufuka. Tutakuwa na miili mikamilifu, isiyokufa. Tunaweza tena kuwaona wapendwa wetu waliokufa. “Roho na mwili vitaungana tena katika umbile lake kamili; vyote kiungo na maungio vitarejeshwa kwenye sura yake sahihi kama vile tulivyo kwa wakati huu” (Alma 11:43).

Yesu Kristo akijitokeza kwa Wanefi

Wanefi wa kale walikuwa na imani katika Mwokozi kabla ya Yeye kuja. Tunaweza kuwa na imani kwamba Mwokozi atakuja tena—Wakati “[sisi] tutakapomwona [Yeye] katika mawingu ya mbinguni amevikwa nguvu na utukufu mkuu” (Mafundisho na Maagano 45:44; ona pia Matendo ya Mitume 1:11). Ni kwa jinsi gani kujua kwamba Yeye atarudi tena kunabadilisha kile utakachofanya leo?

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli” (mkutano wa ibada ya vijana ulimwenguni kote, Juni 3, 2018), Maktaba ya Injili.