Agano Jipya 2023
Kutumia “Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana”


“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarsaa ya Wasichana,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
wavulana wakisoma maandiko

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana

Ni nini madhumuni ya mikutano ya Madarasa Yetu na Akidi Zetu?

Bwana amekupatia wajibu mtakatifu: yeye amekuita kutumikia katika urais wa darasa la Wasichana au urais wa akidi ya Ukuhani wa Haruni. Sehemu ya jukumu lako ni kuongoza na kusimamia mikutano ya darasa lako au akidi siku ya Jumapili. Kufanya hivi, husaidia kuelewa kwa nini tuna mikutano hii.

Mikutano ya darasa la Wasichana na akidi za Ukuhani wa Haruni ni tofauti na madarasa kama vile Shule ya Jumapili au seminari. Katika mikutano ya darasa au akidi, tunajifunza kuhusu kazi ambayo Mungu ametupatia, na tunawapanga washiriki wa darasa au akidi yetu kufanya kazi katika nyumba zetu, Kanisani, na katika jamii yetu. Katika mikutano hii, hatuzungumzii kuhusu kazi—tunafanya mipango ya kutimiza kazi zetu za jeshi la vijana la Bwana, ikijumuisha kusaidia kuikusanya Israeli.

Picha
wasichana wakiwa darasani

Katika mikutano ya darasa au akidi, tunapanga kutimiza wajibu wetu kama sehemu ya bataliani ya jeshi la vijana wa Bwana.

Msisitizo huu kwenye kazi haumaanishi kwamba tunaacha majadiliano juu ya mafundisho tu kwa ajili ya Shule ya Jumapili pekee. Kwa kweli, kujifundisha mafundisho katika mikutano ya madarasa ya wasichana na akidi ya ukuhani wa Haruni ni muhimu—hutusaidia kuimarisha mahusiano yetu na Yesu Kristo, kuelewa mpango wa Baba wa Mbinguni, na kushiriki katika kazi Yao. Tunapojifunza injili kwa pamoja, kweli tunazojifunza zinaweza kubadili mioyo yetu na kutusaidia kujua jinsi ya kutenda zaidi katika njia za kama Kristo. Tunaweza kupokea misukumo kuhusu njia za kuongezeka “katika hekima na kimo, na katika kumpendeza Mungu na wanadamu” (Luka 2:52). Tunapokuwa tumeongoka zaidi kwa Yesu Kristo na injili Yake, tutapata furaha na kuhisi hamu ya kuwasaidia wengine katika mapito ya agano.

Ni Nani Huongoza Mikutano Hii?

Mungu amewaita kama urais wa darasa na wa akidi na kuwapa mamlaka ya kuongoza. Hii ndio kwa nini kila mkutano wa darasa au akidi inapaswa kuongoza na urais wa darasa lako au wa akidi yako. Viongozi watu wazima hawana budi kutoa mwongozo na usaidizi, lakini hawatakiwi kuchukua majukumu yako. Ona sehemu yenye kichwa “Shaurianeni kwa Pamoja” mwanzoni mwa kila muhtasari katika nyenzo hii kwa ajili ya mawazo ya kukusaidia kujua jinsi ya kuongoza mkutano na kutimiza lengo lake lililokusudiwa. Tumia mikutano ya urais kupanga jinsi utakavyoendesha mikutano hii ya Jumapili.

Je, Ni Nani Anapaswa Kufundisha Somo?

Viongozi watu wazima, urais wa darasa au urais wa akidi, au mshiriki mwingine yoyote wa darasa au akidi anaweza kufundisha masomo. Kama urais wa darasa au akidi, shaurianeni na viongozi watu wazima kuhusu nani anatakiwa kupewa jukumu la kufundisha masomo. Kumbukeni kwamba viongozi wenu watu wazima wana mengi ya kutoa. Tafuta kujifunza kutoka kwenye uzoefu na shuhuda zao. Pia kuna uzuri katika kuwaomba vijana kufundisha—kufundisha kunaweza kufanya uongofu wao kuwa wa kina na kuwasaidia wao kujenga mahusiano imara na washiriki wa darasa au akidi. Kwa hivyo wape fursa zinazofaa kufundisha somo lote au sehemu ya somo, lakini ukitilia maanani mahitaji na uwezo wa watu katika darasa lako au akidi. Kwa mfano, viongozi watu wazima wanaweza kufundisha mara nyingi kwenye darasa au akidi pamoja na vijana au pamoja na wale wenye uzoefu mdogo katika kufundisha injili. Wakati vijana wanapoalikwa kufundisha, mzazi au mtu mzima ambaye ni mshauri hana budi kuwasaidia kujiandaa kadiri inavyohitajika.

Wale waliopewa jukumu la kufundisha wanaweza kutumia sehemu yenye kichwa cha habari “Fundisha Mafundisho” katika kila muhtasari kwenye nyenzo hii kuwasaidia wao kujiandaa. Sehemu hii ina mapendekezo kwa ajili ya kufundisha na kujadili mafundisho ya wiki hiyo, lakini walimu hawatakiwi kuhisi kufungwa kwenye mapendekezo haya pekee. Kadiri Roho aongozavyo, walimu wanaweza kutohoa mawazo haya au kutumia ya kwao wenyewe kufundisha katika njia ambayo itatimiza mahitaji vizuri zaidi ya washiriki wa darasa au akidi na kuwasaidia wao kuelewa fundisho.

Je, Tutazijadili Mada Zipi za Injili katika Mikutano Yetu?

Mada ya muhtasari wa kila wiki ni kanuni ambayo imechaguliwa kuendana na usomaji Agano Jipya uliopendekezwa kwa ajili ya wiki hiyo, ipatikanayo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Katika njia hii, majadiliano ya mafundisho katika mikutano ya darasa au akidi yatasaidia katika kile vijana wanajifunza nyumbani.

Hata kama mihutasari itatakiwa kufundishwa katika Jumapili maalum, bado unaweza kuwa na chaguo la kujadili mada zingine za mafundisho kulingana na mahitaji ya darasa lako au akidi yako.

Nyenzo hii inajumuisha mihutasari kwa ajili ya kila wiki wakati mikutano ya madarasa ya Wasichana na akidi ya Ukuhani wa Haruni inapofanyika. Wakati mwingine, unaweza kuhitaji kuruka somo kwa sababu ya mikutano ya kigingi au sababu zingine.

Je, Ni Nini Jukumu la Viongozi Wetu Watu Wazima?

Viongozi wako watu wazima wana jukumu muhimu katika madarasa ya Wasichana na akidi ya Ukuhani wa Haruni. Watakuongoza na kukushauri katika miito yako ya uongozi. Watakusaidia na kukutia moyo wakati unapofanya kazi ya darasa au akidi yako. Watakufundisha mafundisho, na watakuwa baraka kwako kupitia mfano wao, uzoefu, na ushuhuda.

Chapisha