Agano Jipya 2023
Januari 8. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwabariki Wengine na Ushuhuda Wangu juu ya Yesu Kristo? Mathayo 1; Luka 1


Januari 8. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwabariki Wengine na Ushuhuda Wangu juu ya Yesu Kristo? Mathayo 1; Luka 1,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

Januari 8. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwabariki Wengine na Ushuhuda Wangu juu ya Yesu Kristo?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
Kulingana na Neno Lako, na Elspeth Young

Mariamu alitoa ushuhuda wa nguvu juu ya misheni ya Kristo (ona Luka 1:46–55). Kulingana na Neno Lako, na Elspeth Young

Januari 8

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwabariki Wengine na Ushuhuda Wangu juu ya Yesu Kristo?

Mathayo 1; Luka 1

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja au mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org) Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Tulijadili nini wakati uliopita, na ni mialiko gani au kazi gani zilitolewa? Tumefanya nini kushughulikia mialiko hiyo au kazi hizo?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Tunaweza kufanya nini au kusema nini ili kuwafikia wale wanaoweza kuwa wanahisi kuwa wapweke au wako mbali na Baba wa Mbinguni?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Yesu Kristo?

  • Unganisha familia milele. Ni mawazo gani tunaweza kushiriki mmoja na mwingine kuimarisha familia zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kama Wayahudi wengi waaminifu wa wakati wake, Mariamu alikuwa kwa hamu kweli anatamani kwa ujio wa Masiya. Baada ya kujifunza kutoka kwa malaika kwamba kusubiri kulikuwa karibu kuisha—na kwamba yeye angekuwa mama ya Mkombozi aliyeahidiwa—Mariamu alitoa ushuhuda mzuri wa “Mungu Mwokozi wangu.” Ushuhuda huu umeandikwa katika Luka 1:46–55, na ni pendwa kwa Wakiristo kote ulimwenguni. Unaposoma mistari hii, fikiria kuhusu watu katika darasa au akidi yako. Wao, kama vile Mariamu, wanajiandaa kwa ujio wa Yesu Kristo—wakati huu, kwa Ujio wa Pili Wake mtukufu. Na pia kama Mariamu, shuhuda zao zinaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu juu ya imani ya wale walio karibu nao.

Ni kwa jinsi gani vijana unaowafundisha wanahisi kuhusu Yesu Kristo? Ni kwa jinsi gani shuhuda zao juu Yake zinawabariki wengine? Unapojiandaa kufundisha, ungeweza pia kujifunza 2 Nefi 25:23–26 na ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Tunazungumza Juu ya Kristo” (Liahona, Mei 2020, 88–91).

Jifunzeni Pamoja

Njia nzuri ya kuwasaidia vijana kufikiria kuhusu shuhuda zao juu ta Yesu Kristo ni kuuchunguza ushuhuda wa Mariamu katika Luka 1:46–55. Pengine wangeweza kushiriki mmoja na mwingine virai ambavyo vinaelezea kile Mariamu alichoamini na kuhisi kuhusu Mwokozi. Ni vipi kati ya virai hivi pia vinavyoelezea jinsi tunahisi kumhusu Yeye? Kwa mfano, ni nini husababisha roho zetu “[kufurahia] katika Mungu”? (mstari 47). Je, ni “mambo gani makuu” Yeye aliyokutendea? (mstari wa 49). Ni kwa jinsi gani Yeye ameonyesha uweza Wake katika maisha yetu? (ona mstari wa 51). Mawazo ya shughuli hapo chini yangeweza kuongoza kwenye mazungumzo kuhusu jinsi shuhuda zetu za Kristo zinaweza kuwabariki wengine.

  • Ujumbe wa Neil L. Andersen “Tunazungumza Juu ya Kristo” husaidia kuelezea kwa nini tunapaswa kuongea wazi zaidi juu ya Mwokozi—na jinsi tunaweza kufanya hivyo. Mngeweza kusoma sehemu za ujumbe wa Mzee Andersen pamoja. Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kujadili sababu yeye alitoa za kushiriki shuhuda zetu juu ya Yesu Kristo na ushauri wake wa kufanya hivyo Ni mambo gani mahsusi tunaweza kuongea juu ya Kristo kwa uwazi zaidi?

  • Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunajua kweli muhimu kuhusu Yesu Kristo ambazo tunaweza kushiriki. Ni kwa jinsi gani utawasaidia vijana kufikiria kweli hizi? Ungeweza kuwaomba wajifunze “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” mmoja mmoja au katika makundi, wakitafuta majibu ya swali “Ni kweli gani kuhusu Mwokozi zilizo na maana maalumu kwetu?” Waombe washiriki kweli walizopata na waelezee kwa nini kweli hizi ni muhimu kwao. Wangeweza kushiriki maandiko na uzoefu wao wenyewe wanapofanya hivyo. Wangeweza kisha kujadili ni kweli zipi kuhusu Mwokozi wangeweza kuhishiriki kwenye vyombo vya kijamii, na rafiki anayehangaika na ushuhuda au mtu fulani ambaye si muumini wa Kanisa letu.

  • Kama nyongeza ya Luka 1:46–55, maandiko yana vifungu vingi ambavyo vingeweza kuwatia moyo kushiriki kile wanachojua kuhusu Yesu Kristo. Baadhi ya mifano imeorodheshwa katika “Nyenzo Saidizi.” Fikiria kusoma maandiko haya pamoja. Yanatufundisha nini sisi kuhusu jinsi ya kushiriki shuhuda zetu juu ya Yesu Kristo na wengine? Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hizi? Washiriki wa darasa au akidi wangeweza pia kushiriki kile ambacho wamejifunza kutoka kwa watu ambao wanawajua ambao wanashiriki imani yao katika Yesu Kristo bila uoga.

Picha
wasichana wakijifunza maandiko

Tunapojifunza ili kumjua na kumpenda Mwokozi, tunapata njia za kushiriki shuhuda zetu juu Yake.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kuuliza maswali ambayo yanawatia moyo wanafunzi kutoa ushuhuda kunaweza kuwa njia yenye nguvu ya kumwalika Roho. Ungeweza kuuliza maswali kama “Ni kwa njia gani umekuja kufahamu kwamba Yesu Kristo alifanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zako?” au “Ni kwa jinsi gani umekuja kuthamini yale Mwokozi alifanya kwa ajili yetu kule Gethsemane?”

Chapisha