Agano Jipya 2023
Januari 22. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Ni Nuru katika Maisha Yangu? Yohana 1


Januari 22. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Ni Nuru katika Maisha Yangu? Yohana 1,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni na Darasa la Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

Januari 22. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Ni Nuru katika Maisha Yangu?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
Ninyi ni Nuru ya Ulimwengu, na Simon Dewey

Ninyi ni Nuru ya Ulimwengu, na Simon Dewey

Januari 22

Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Ni Nuru katika Maisha Yangu?

Yohana 1

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Je, ni uzoefu gani ya hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Je, ni akina nani wanahitaji msaada wetu na sala zetu? Je, ni nini tunahisi kuvutiwa kukifanya ili kuwasaidia?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa wanafamilia au marafiki ambao hawashiriki imani yetu?

  • Unganisha familia milele. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha upendo zaidi na ufadhili kwa familia zetu na kuleta tofauti chanya katika nyumba zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Mtume Yohana alianza Injili yake kwa kumlinganisha Yesu Kristo na nuru ambayo “inang’aa gizani” (Yohana 1:5). Washiriki wengi wa darasa lako au akidi wanakua katika nyakati za giza la kiroho. Lakini pia ni wakati ambapo “nuru ya ajabu” ya Mwokozi inapatikana kuwasaidia wao kuona kwa uwazi na kupata njia zao (1 Petro 2:9).

Unaposoma Yohana 1 wiki hii, tafakari kwa nini nuru ni muhimu sana na jinsi Mwokozi ni nuru katika maisha yako (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Yohana 1:1–34 [katika kiambatisho cha Biblia]). Ni kwa jinsi gani nuru Yake ingeweza kuwabariki wale unaowafundisha? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwahamasisha wao kutembea katika nuru Yake? Ili kukusaidia kutafakari maswali haya, ungeweza kujifunza Mafundisho na Maagano 88:5–13, 67; 93:2–9 na ujumbe wa Dada Sharon Eubank “Kristo: Nuru Ambayo Huangaza Gizani” (Liahona, Mei 2019, 73–76).

Jifunzeni Pamoja

Mara nyingi inakuwa msaada kuanzisha mazungumzo kwa kuwapa darasa au akidi nafsi ya kuongea kuhusu kile wamekuwa wakijifunza kutoka kwenye kujifunza maandiko kwao. Kwa mfano, wiki hii ungeweza kuwaomba washiriki neno au kirai kutoka katika Yohana 1:1–17 ambacho kinawafundisha wao kitu fulani kuhusu Mwokozi. Acha wazungumze kuhusu kwa nini walichagua neno au kirai chao na kinafundisha nini kuhusu Yesu Kristo. Shiriki nao jinsi Yesu Kristo ni nuru katika maisha yako. Shughuli hapa chini zinaweza kukusaidia kuendelea na mjadala.

  • Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema nuru ya Kristo, labda mshiriki wa darasa au akidi angeweza kushiriki vile anahisi kuwa katika gizani. Kuna hadithi ambayo ingeweza kusaidia hapo mwanzoni wa ujumbe wa Mzee Timothy J. Dyches “Nuru Huambatana na Nuru” (Liahona, Mei 2021, 112–15). Je, kwa nini watu wakati mwingine wanaogopa giza? Kwa nini tunahitaji nuru? Kwa nini Yesu Kristo Anaitwa Nuru ya Ulimwengu? Ungewaomba vijana kujifunza ujumbe wa Mzee Dyches kuanzia na “Naomba nipendekeze kwamba, pengine, huu ni wakati wa kujiuliza mwenyewe.” Wangeweza kutafuta kile tunachoweza kufanya ili kuleta nuru ya Mwokozi zaidi katika maisha yetu.

  • Maandiko yaliyoorodheshwa kwenye “Nyenzo Saidizi” yanaweza kusaidia darasa lako au akidi yako kuelewa nuru ambayo Yesu Kristo anatoa. Ungeweza kusoma na kujadili chache katika seti ya kwanza ya maandiko kama darasa. Kisha andika Ni kwa jinsi gani tunaweza kuleta nuru ya Mwokozi maisha yetu? Ubaoni, na waalike vijana kuorodhesha maswali wanayopata katika seti ya pili ya maandiko. Ungeweza kuwaweka vijana katika majozi na kuwaomba wao kushiriki na kila mmoja jinsi Yesu Kristo amekuwa nuru katika maisha yao.

  • Dada Sharon Eubank alisema, “Mojawapo ya mahitaji ya msingi tunayo ili kukua ni kukaa kama umeunganika na chanzo chetu cha nuru—Yesu Kristo” (“Kristo: Nuru Ambayo Huangaza Gizani,” 73). Ungeweza kuonyesha hili kwa somo la vyombo—pengine kuonyesha tochi au chombo tamba na kuzungumza kwa nini chanzo cha nguvu ni umeme ni muhimu. Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kisha kupitia tena ujumbe wa Dada Eubank, wakitafuata njia Shetani hujaribu “kukata umeme wetu.” Ni kwa jinsi gani tunadumisha muunganiko na Yesu Kristo? Ni ushauri gani tunaoupata katika ujumbe wa Dada Eubank?

  • Nyimbo kama vile “The Lord Is My Light” na “Lead, Kindly Light” (Nyimbo, na. 89, 97) zinashuhudia kwamba Yesu Kristo ni nuru yetu. Fikiria kuimba hizi (au zingine mnazojua) pamoja na kutambua maneno au virai ambavyo vinatufundisha sisi jinsi Yesu Kristo ni kama nuru. Je, ni kwa namna gani wengine walileta nuru ya Mwokozi katika maisha yetu? Ni kwa insi gani tunaweza kushiriki nuru Yake na wengine?

Picha
Zawadi ya Nuru, na Eva Timothy

Zawadi ya Nuru, na Eva Timothy

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Unapotazama kila kitu kinachofanyika maishani mwa washiriki wa darasa lako au akidi yako, utaona fursa nzuri sana za kufundisha. Maoni ambayo wanafunzi hutoa au maswali ambayo wao huuliza yanaweza kuelekeza kwenye nyakati za kufundisha.

Chapisha