Agano Jipya 2023
Februari 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuboresha Kuabudu Mungu Kwangu? Yohana 2–4


“Februari 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuboresha Kuabudu Mungu Kwangu? Yohana 2–4,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Februari 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuboresha Kuabudu Mungu Kwangu?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Kisimani, na Crystal Suzanne

Kisimani, na Crystal Suzanne

Februari 12

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuboresha Kuabudu Mungu Kwangu?

Yohana 2–4

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Je, ni kwa jinsi gani tumekaribia Mwokozi? Je, ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni nani amekuwa katika akili zetu karibuni? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaida watu binafsi?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, tunaweza kujibu maswali ya marafiki zetu kuhusu Kanisa katika njia ambayo inaimarisha imani yao katika Mwokozi?

  • Unganisha familia milele. Ni njia zipi tunazoweza kuunganika vyema na wanafamilia wengine kama vile kina babu na binamu zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Mwanamke Msamaria aliyelezewa katika Yohana 4 labda alienda kisimani kuteka maji kila mara. Lakini safari hii ilikuwa tofauti. Alikutana na mwanaume Myahudi ambaye alimuomba maji ya kunywa. Hiyo peke yake ilikuwa sio kawaida kwa sababu Wayahudi kwa kawaida hawakuwa na miingiliano na Wasamaria. Lakini kuna kitu kingine kisicho cha kawaida kuhusu mtu huyu. Akiona kwamba Yeye lazima alikuwa nabii, alimuuliza Yeye maswali kuhusu kumwabudu Mungu. Ilikuwa inakubalika kumwabudu Mungu hapo katika Samaria? Au lazima watu waliabudu katika Yerusalemu, kama vile Wayahudi walivyodai? (Ona Yohana 4:19–20). Mtu huyu alielezea kwamba pale tunapoabudia sio muhimu kama vile tunavyoabudu: “Waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” (Yohana 4:23). Kisha mtu yule akamwambia Yeye alikuwa ni nani—Yeye alikuwa Kristo, Mwokozi wa ulimwengu (ona Yohana 4:25–26).

Je, vijana unaowafundisha wanaelewa kile inamaanisha kumwabudu Baba wa Mbinguni? Kama nyongeza ya kuabudu kanisani (ona Mafundisho na Maagano 59: 9–10), ni fursa gani zingine walizonazo za kumwabudu Yeye, ikijumuisha zile wanaweza wasitambue kama kuabudu? Nyenzo zifuatazo zinaweza kukusaidia kuandaa kuwafunza wao kuhusu jinsi ya kuboresha kumwabudu Mungu kwao: Zaburi 95:1–7; Mathayo 4:8–10; Alma 32:4–11; Mafundisho na Maagano 20:17–19; 93:19–20, na ujumbe wa Askofu Dean M. Davies “Baraka za Kuabudu” (Liahona, Nov. 2016, 93–95).

Jifunzeni Pamoja

Ili kuanza mjadala kuhusu kuboresha kuabudu, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa au akidi kibinafsi kupitia tena Yohana 4:19–26 na kuandika majibu yao kwa maswali kama haya: Kwa nini ninamwabudu Mungu? Inamaanisha ni kwangu kumwabudu Mungu? Ingeweza pia kuwa msaada kupitia tena maelezo chini ya “Kuabudu” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Baada ya wao kuwa na muda wa kutafakari maswali haya, waalike kushiriki mawazo yao. Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia wao kupokea mnong’ono wa Roho Mtakatifu.

  • Washiriki wa darasa au akidi yako walipata umaizi kuhusu kile inamaanisha kumwabudu Mungu. Ungeweza kuwaomba wao kushiriki uzoefu wakati walihisi walikuwa wanamwabudu Mungu. Vifungu vya maandiko kama vifuatavyo vinaweza kuongeza uelewa wao na kuwapa mawazo kuhusu jinsi ya kufanya kumwabudu Mungu kwao kuwa na maana zaidi: Zaburi 95:1–7; Mathayo 4:8–10; Alma 32:4–11; Mafundisho na Maagano 20:17–19; 93:19–20. Wangeweza pia kujadili kauli ua Mzee Bruce R. McConkie katika “Nyenzo za Saidizi.”

  • Ili kuwasaidia vijana kuboresha kumwabudu Mungu kwao, fikiria kuandika vichwa hivi ubaoni: Nani, Kwa nini, Wapi, na Vipi. Waombe wao kupitia tena maandiko yaliyoorodheshwa katika “Kuabudu” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures,ChurchofJesusChrist.org), wakitafuta mistari ambayo inawasaidia wao kuelewa nani, kwa nini, wapi, na vipi tunapaswa kuabudu. Wanapopata mstari husika, waalike waujadili katika darasa au kuandika marejeo chini ya vichwa vifaavyo. Wahimize kushiriki uzoefu wakati walihisi kuwa karibu na Mungu kupitia kuabudu.

  • Ujumbe wa Askofu Dean M. Davies “Baraka za Kuabudu” una mifano ya watu wakimwabudu Mungu. Pengine mngeweza kusoma pamoja sehemu hii “Kuabudu ni Nini?” Kisha kila mtu angeweza kupitia tena mojawapo ya mifano ya watu wakiabudu inayopatikana katika sehemu tatu zifuatazo za ujumbe huu. Ni nini kila mfano unatufundisha kuhusu kumwabudu Mungu? Ni nini sehemu ya mwisho ya ujumbe huu inafundisha kuhusu baraka ambazo huja kutokana na kumwabudu Mungu kwa bidii? Je, unashawishika kufanya nini ili kuboresha kumwabudu Mungu kwako?

kijana akisoma

Kuabudu hujumuisha kujifunza maandiko na mambo mengine ambayo yanaonyesha bidii na upendo kwa ajili ya Mungu.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

  • Elements of Worship,” Teachings of Presidents of the Church: David O. McKay (2003), 29–37

  • Donald L Hallstrom, “Uongofu wa Watoto wa Mungu” (Seminaries and Institutes of Religion broadcast, Jun. 13, 2017), broadcasts.ChurchofJesusChrist.org

  • Mzee Bruce R, McConkie alifundisha: “Kuabudu halisi na kamili ni kufuata hatua za Mwana wa Mungu; ambazo ni kushika amri na kutii mapenzi ya Baba kwa kiwango hicho ambacho tunasonga kutoka neema hadi neema mpaka tunapotukuka katika Kristo kama vile Yeye alivyo katika Baba Yake. Ni zaidi ya sala na mahubiri na wimbo. Ni kuishi na kufanya na kutii. Ni kuiga maisha ya Mfano mkuu” (“How to Worship,” Ensign, Desemba 1971, 130; herufi kubwa zimesasishwa).

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mafundisho yanayopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho yana nguvu ya kubadilisha mioyo na kuongeza imani. Wakati wewe na wale unaofundisha “wangejaribu matokeo ya uwezo wa neno la Mungu,” utapata kwamba lina “maelekezo makubwa ya kuongoza watu kufanya yale ambayo ni haki” (Alma 31:5).