Agano Jipya 2023
Februari 26. Ni kwa Jinsi Gani Mafundisho ya Mwokozi Yananisaidia Kufanya Hukumu ya Haki? Mathayo 6–7


“Februari 26. Ni kwa Jinsi Gani Mafundisho ya Mwokozi Yananisaidia Kufanya Hukumu ya Haki? Mathayo 6–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Februari 26. Ni kwa Jinsi Gani Mafundisho ya Mwokozi Yananisaidia Kufanya Hukumu ya Haki?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
Yesu na mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi

Februari 26

Ni kwa Jinsi Gani Mafundisho ya Mwokozi Yananisaidia Kufanya Hukumu ya Haki?

Mathayo 6–7

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni mada gani uaskofu umejadili katika mikutano ya baraza la vijana la kata yenu? Tunaweza kufanya nini kama darasa au akidi kulingana na umuhimu wa mijadala hiyo?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafikia watu katika njia za kama Kristo wakati tunaona hitaji na hatujui cha kusema?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, tumepata nini kutoka katika injili ya Yesu Kristo ambacho kinatuletea shangwe? Je, tunawezaje kushiriki shangwe hiyo na wengine?

  • Unganisha familia milele. Tunafanya nini ili kupata majina ya mababu zetu ambao wanahitaji ibada za hekaluni? Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kupata majina ya mababu zao?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kuna mwelekeo katika kila mmoja wetu—kama matokeo ya asili yetu ya kuanguka—kuwahukumu wengine, wakati mwingine pasipo haki au kiburi. Lakini Joseph Smith alifundisha, “Msihukumu pasipo na haki, ili nanyi msihukumiwe: lakini toeni hukumu ya haki, (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 7:1 [katika Mathayo 7:1, tanbihi a]). Tafakari jinsi ushauri huu unaweza kukubariki wewe na wale unaowafundisha. Mwokozi alionyesha kwa mfano kile Yeye alichomaanisha na “hudumu ya haki.” Kwa mfano, fikiria jinsi Yeye alivyomtendea mwanamke ambaye alifanya uzinzi. Yeye hakumhukumu, bali Yeye pia hakuruhusu dhambi yake. Alimwambia “enenda zako; wala usitende dhambi tena.” (Yohana 8:11). Je, tunajifunza nini kuhusu kuhukumu kwa haki kutoka kwa Mwokozi?

Unapotafakari jinsi utakavyowasaidia vijana kuelewa hukumu ya haki, ungeweza kujifunza Mathayo 7:1–2 na ujumbe wa Mzee Lynn G. Robbins “Mwamuzi wa Haki” (Liahona, Nov. 2016, 96–98).

Jifunzeni Pamoja

Ungeweza kuanza majadiliano kuhusu kuhukumu kwa haki kwa kuwaomba washiriki wa darasa au akidi kufikiria wakati walipohisi kuhukumiwa kimakosa na wengine. Je, walihisi vipi? Tunajifunza nini kuhusu kuhukumu kutokana na mafundisho ya Mwokozi katika Mathayo 7:1–5? (Ona Tafsiri ya Joseph Smith katika tanbihi 1a). Kirai “hukumu ya haki” kingeweza kumaanisha nini? Ungeweza kujadili mistari hii na kuwaalika washiriki wa darasa au akidi kusema kila mstari kwa maneno yao wenyewe. Shughuli kama zifuatazo pia zinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuhukumu kwa haki.

  • Mafundisho ya Mwokozi katika Mathayo 6–7 yanaweza kutusaidia kutoa hukumu ya haki? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kugundua mafundisho haya, ungeweza kumpa kila mmoja wao moja ya vifungu vifuatavyo ili kutafakari: Mathayo 6:14–15; 7:3–5; 7:12; 7:15–20. Maneno ya Mwokozi katika mistari hii yanapendekeza nini kuhusu kile inamanisha kuhukumu kwa haki? Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Mwokozi katika Yohana 8:1–11 na Mathayo 9:10–13? Je, ni tofauti gani tunaiona kati ya njia ambayo Mwokozi anatuhukumu na njia tunayohukumiana mara kwa mara?

  • Kwa sababu sisi sote tuna haki ya kujiamulia, sharti kila mara tutoe hukumu kuhusu kile tutafanya na kile hatutafanya. Kama wafuasi wa Mwokozi, tunajitahidi tusihukumu au kuwakosoa watu wengine. Ili kuwasaidia vijana kuelewa tofauti, shiriki nao kauli ya Rais Dalllin H. Oaks katika “Nyenzo Saidizi.” Kama darasa au akidi, fanyeni kazi pamoja kufikiria mifano ya kuhukumu hali—kama vile shughuli, tukio, au mazungumzo—badala ya kumhukumu mtu anayehusika. Kwa nini ni bora kuhukumu hali badala ya mtu? Vijana wanaweza kuwa na maswali mengine kuhusu kuhukumu kwa haki (ona mifano katika “Nyenzo Saidizi). Jadilini maswali yao pamoja mkitumia taarifa chini ya “Nyenzo Saidizi” kupata majibu. Waalike vijana kushiriki kile wanachohisi kuvutiwa kufanya kwa sababu ya kile wanachojifunza.

  • Katika ujumbe wake katika mkutano mkuu “Kukuza Hukumu Nzuri na Kutowahukumu Wengine” (Liahona, May 2010, 103–5), Mzee Gregory A. Schwitzer alisimulia hadithi mbili—ya Martha rafiki ya Yesu na mtu Mzee Schwitzer alimusaidia. Hadithi hizi zinafundisha nini kuhusu jinsi tunavyopaswa kuwaona wengine na kuwatendea wengine? Ni kanuni zipi zinaweza kutusaidia kuwa zaidi kama Kristo na kuhukumu kwa haki? Video “Looking through Windows” na “Judging Others? Stop It!” (ChurchofJesusChrist.org) zingeweza kutoa umaizi wa ziada.

Picha
vijana wakubwa wakiongea

Tunapojifunza kuwa zaidi kama Kristo, tunaweza kuhukumu kwa haki zaidi.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

  • Mifano ya maswali kuhusu kuwahukumu wengine: “Nimefunzwa kuwachagua marafiki zangu kwa makini. Lakini ninawezaje kufanya hivyo bila kuwahukumu watu? “Mimi ninapojaribu kuishi injili, nadaiwa kuwa mwenye kuhukumu. Ni kwa jinsi gani ninaweza kuwa mkweli kwa kile ninaamini na kuonyesha upendo kwa wale tusiokubaliana?

  • 1 Samweli 16:7; Moroni 7:12–19; Mafundisho na Maagano 11:12

  • Mada za Injili, “Kuwahukumu Wengine,” topics.ChurchofJesusChrist.org

  • Rais Dallin H. Oaks alifundisha: “Pale inapowezekana tutajiepusha na kuwahukumu watu na tuhukumu hali tu. Hii ni muhimu pale tunapojaribu kutenda juu ya viwango tofauti na wengine ambao ni lazima tutangamane nao—nyumbani, kazini, au katika jamii. Tunaweza kuweka na kutenda kwa viwango vya juu kwa ajili yetu wenyewe au nyumbani bila kuwashtumu wale wanaofanya vivyo hivyo” (“‘Usihukumu’ na Kuhukumu,” Ensign, Agosti 1999. 11).

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Juhudi zako zinapaswa kuhimili juhudi za wazazi. Shirikiana na wazazi wa vijana juu ya kile unachowafundisha. Shauriana nao ili wajifunze kuhusu mahitaji ya vijana katika darasa lako na njia bora za kuweza kusaidia katika kukidhi mahitaji hayo.

Chapisha