“Machi 12. Ni kwa Jinsi Gani Mwokozi Anaweza Kunisaidia Kushinda Hofu Yangu? Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Machi 12. Ni kwa Jinsi Gani Mwokozi Anaweza Kunisaidia Kushinda Hofu Yangu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Machi 12
Ni kwa Jinsi Gani Mwokozi Anaweza Kunisaidia Kushinda Hofu Yangu?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu?
-
Kuwajali wenye mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana katika mambo tunayopitia?
-
Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia tekinolojia kama chombo cha kushiriki injili?
-
Unganisha familia milele. Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja kwa Kristo?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Sura ya 5 katika kitabu cha Marko imeandikwa kwamba watu watatu walimjia Yesu ambao walikuwa na sababu zote za kuogopa. Mtu aliyekuwa na “pepo mchafu” alikabiliwa na maisha ya upweke, akiishi “ makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe” (Marko 5:2, 5). Yairo, mtawala wa sinagogi, alikuwa na hofu ya kumpoteza binti yake, ambaye alikuwa “yu katika kufa” (Marko 5:23). Na mwanamke mwenye “kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili” hakuponywa baada ya “amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo” kwa matabibu wengi” (Marko 5:25–26). Kila mtu unayemfundisha ni wa kipekee na anakumbana na hofu zake mwenyewe. Lakini kama vile Mwokozi alivyowafurusha mapepo wachafu, kuwafufua wafu, na kuponya maradhi makali, Yeye hutusaidia wakati tuna hofu. Ushauri wake kwa Yairo una nguvu kubwa katika maisha yetu leo: “Usiogope, amini tu” (Marko 5:36).
Unapojiandaa kufundisha, fikiria kujifunza ujumbe wa Mzee Ronald A, Rasband “Msifadhaike” (Liahona, May 2018, 18–21) na ujumbe wa Dada Lisa L. Harkness“Nyamaza, Utulie” (Liahona, ([2020], 80–82).
Jifunzeni Pamoja
Ungeweza kualika washiriki wa darasa au akidi kufanya muhtasari wa hadithi iliyopo katika Marko 5 ya Yesu akimwalika Yairo “usiogope” (ona mstari wa 22–24, 35–43), au mngeweza kupitia tena hadithi hii kama kikundi. Ungeweza kufanya vivyo hivyo kwa hadithi zingine katika sura hii—mtu aliyekuwa na pepo mchafu na mwanamke aliyetokwa na damu. Ni kwa jinsi gani hali za kuogofya hizi ni sawa na zile tunazokabiiana nazo katika maisha yetu? Je, tunajifunza nini kutoka kwenye hadithi hizi kuhusu Mwokozi na jinsi tunaweza kutafuta msaada Wake? Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia vijana kuongeza imani yao katika Yesu Kristo na kujifunza kuufuata ushauri Wake: “Usiogope, amini tu” (Marko 5:36).
-
Mwaliko wa Bwana wa usiogope, umerudiwa kote katika maandiko, utawabariki vijana wakati wanapokuwa na hofu. Waalike wao kusoma maandiko katika “Nyenzo Saidizi” na utengeneze bango wanaloweza kutundika nyumbani—au bango la kidigitali ambalo wangeshiriki mtandaoni—kulingana na maandiko waliyosoma. Wanaposhiriki kile walichotengeneza na kila mmoja, waalike wao pia washiriki kile walichojifunza ambacho kinaweza kuwasaidia wanapokuwa na hofu. Ni lini ambapo Mwokozi alitusaidia wakati wa hofu?
-
Fikiria kuonyesha picha ya Mwokozi akituliza dhoruba, moja kama ile ya toleo la digitali la ujumbe wa Dada Lisa L. Harkness “Nyamaza, Utulie” (ona pia Kitabu cha Sanaa za Injili [2009], na, 40). Kisha wewe au mtu uliyempangia angeweza kushiriki tukio la Mwokozi akituliza dhoruba kutoka katika Marko 4:35–41 au kutoka katika ujumbe wa Dada Harkness. Ni kwa jinsi gani wakati mwingine sisi tuko kama wale walio katika meli? Tunajifunza nini kutoka kwenye hadithi hii kuhusu jinsi Mwokozi anavyotusaidia tunapokuwa na hofu? Waalike vijana wachache kupitia tena ujumbe wa Dada Harkness, wakitafuta virai au sentesi ambazo zinawasaidia wao kuwa na imani kuu zaidi katika Yesu Kristo. Wanaweza kuandika hizo ubaoni. Ni kwa jinsi gani imani yetu katika Mwokozi hutusaidia wakati ambapo si mapenzi Yake kutuliza dhoruba za maisha yetu?
-
Nyimbo kadhaa zinamsifu Mwokozi kwa ajili ya faraja Yake na nguvu nyakati za changamoto na taharuki, kama vile “I Need Thee Every Hour” au “Abide with Me!” ((Nyimbo, namba. 98, 166). Kisha mngeweza kuimba au kusoma chache ya hizo pamoja, mkitafuta jinsi Mwokozi anaweza kutusaidia.
-
Hofu na wasiwasi ni kawaida tunapokabiliana na changamoto za maisha. Kwa wengine, hisia hizi zinaweza kulemaza. Darasa lako au akidi ingeweza kufaidika kutokana na mjadala kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kuwasaidia wale wanaotaabika na wasiwasi wa viwango tofauti. Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kupitia tena ujumbe wa Mzee Ronald A. Rasband “Msifadhaike” au ujumbe wa Mzee Erich W. Kopischke “Kuzungumzia Afya ya Akili” (Liahona, Nov. 2021, 36–38), wakitafuta kweli ambazo zina maana sana kwao na kushiriki kile walichopata. Wahimize vijana kuzungumza na mzazi au kiongozi wanayemuamini au watembelee mentalhealth.ChurchofJesusChrist.org kama wanahitaji msaada.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.