87
Kaa Nami!
Kwa unyenyekevu
1. Kaa nami! Kwani kumekuchwa;
Usiniache gizani, Bwana!
Wanaposhindwa wasaidizi,
Auni wa kweli, kaa nami!
2. Siku zinayoyoma haraka.
Duniani raha hufifia.
Naona mabadiliko mengi;
Ewe Mwaminifu, kaa nami!
3. Kila saa ninakuhitaji.
Nani atamshinda Shetani?
Mwimo wangu, mwingine hakuna,
Kila hali kaa nami, Bwana!
Maandishi: Henry F. Lyte, 1793–1847
Muziki: William H. Monk, 1823–1889