9
Lo! Mlimani Kumora
Kwa kutafakari / Kwa ari
1. Malaika wa juu
Kavunja kimya chake;
Kashuka kwenye mbingu,
Haya maneno yake:
Lo! Mlimani Kumora
Maandiko yamefichwa.
Lo! Mlimani Kumora
Maandiko yamefichwa.
2. Na kwa muda mrefu
Alificha Moroni;
Akingojea Mungu
Aitolee amri.
Itafunuliwa tena
Kufanya njia ya Bwana.
Itafuunuliwa tena
Kufanya njia ya Bwana.
3. Inazungumzia
Uzao wa Yusufu
Na yale mataifa,
Yaliyo mapotevu.
Na utimilifu huo,
Wa injili yake Kristo.
Na utimilifu huo
Wa injili yake Kristo.
4. Sasa ndiyo wakati,
Uliotarajiwa;
Ulimwengu utii,
Giza litatoweka.
Kitabu kifunguliwe,
Duniani kiangaze.
Kitabu kifunguliwe,
Duniani kiangaze.
5. Tazama Israeli
Watakusanywa kwao
Watajenga kwa mali
Yerusalemu yao,
Na Sayuni itang’aa,
Ukweli ikieneza.
Na Sayuni itanga’a,
Ukweli ikieneza.
Maandishi: Parley P. Pratt, 1807–1857
Muziki: John E. Tullidge, 1806–1873