165
Maisha Yaliyo Mema
Kwa kutafakari
1. Maisha yaliyo mema
Huakisi wako wema;
Unatubariki, Mungu,
Kupitia ndugu zetu.
2. Ni zawadi gani kubwa,
Ni zawadi gani bora,
Kama walio na Yesu
Kukuza imani zetu.
3. Na rafiki kama huyu,
Mioyoni atadumu
Kutukumbusha vizuri
Kukaribia mbinguni.
4. Twakushukuru Mwokozi
Kwa marafiki wazuri,
Walio waaminifu,
Na wanaokuabudu.
Maandishi: Karen Lynn Davidson, 1943–2019. © 1985 IRI
Muziki: A. Laurence Lyon, 1934–2006. © 1985 IRI