107 Nje ya Yerusalemu Kwa unyenyekevu 1. Nje ya Yerusalemu Kilimani kule, Alisulubiwa Kristo Kuokoa sote. 2. Hatuwezi kuelewa Yake maumivu, Aliteswa, twaamini, Kwa ajili yetu. 3. Hapakuwa na mwingine, Wa kulipa deni. Yeye kafungua lango Tufike mbinguni. 4. Alitupenda kwa dhati! Nasi tumpende! Damu yake tusadiki, Na tumfuate. Maandishi: Cecil Frances Alexander, 1818–1895 Muziki: John H. Gower, 1855–1922 Yohana 19:16–20 Waebrania 13:12