95
Tunaposhiriki Nembo
Kwa hamasa
1. Tunaposhiriki nembo
Kwa jina la Yesu Kristo,
Sote na tuihakiki
Mioyo kama ni safi.
2. Kristo damu alimwaga,
Golgotha ilimwagika,
Kifungo kutunusuru
Na kuepuka adhabu.
3. Hivyo Yesu alikufa
Ili haki kutimia,
Ili watu tuwe huru
Na kifo pia kuzimu.
4. Lakini tutafufuka,
Na tutaishi daima,
Hatutateswa na kifo,
Tutatawala na Kristo.
Maandishi: John Nicholson, 1839–1909
Muziki: Alexander Schreiner, 1901–1987. © 1948 IRI
Jina la tuni: AEOLIAN