33
Sifa Kwa Bwana, Mwenyezi
Kwa shangwe
1. Sifa kwa Bwana, Mwenyezi, Mfalme wa mbingu!
O! Nafsi msifu aliye wokovu wangu!
Jumuika
Kwa zeze na kinanda,
Imbeni kwa kumwabudu!
2. Sifa kwa Bwana! Atawala kwa utukufu.
Kwenye mabawa huchukua Watakatifu.
Hujaona
Mahitaji kakupa
Alichokiweka wakfu?
3. Sifa kwa Bwana, mlinzi akuwezeshaye.
Hakika fadhila yake daima i nawe.
Tafakari
Uwezo wa Mwenyezi,
Rafiki akupendaye.
4. Sifa kwa Bwana! O! Nafsi yangu umwabudu!
Wote ungana na Abrahamu kumwabudu!
Na “amina!”
Zijumlishe sifa,
Sasa tunapoabudu.
Maandishi: Joachim Neander, 1650–1680; yalitafsiriwa na Catherine Winkworth, 1829–1878
Muziki: Kutoka Stralsund Gesangbuch, 1665; umepangiliwa na William S. Bennett, 1816–1875, na Otto Goldschmidt, 1829–1907