124
Bwana, Pokea Uliko
Kwa kushangilia
1. Bwana, pokea uliko
Kila anayetubu,
Azaliwaye kwa maji
Na roho wako, Mungu.
Wafariji na ongoza
Maisha ya vijana;
Na neno lako tukufu
Liwape maarifa.
2. Hamjui ndiye Mungu?
Na akawa shahidi,
Kwamba njia ni nyembamba
Irudiyo mbinguni.
Sikia habari njema;
“Njoo, unifuate
Katika ufalme wangu,
Na uishi milele.”
3. Ukweli umerejeshwa:
Ibada takatifu,
Kwa agano ziokoe
Milele wanadamu!
Watu wote mfurahi!
Watu wote muimbe!
Waliokufa wasifu
Mungu wetu Mfalme!
Maandishi: Mabel Jones Gabbott, 1910–2004. © 1948 IRI
Muziki: Alexander Schreiner, 1901–1987. © 1948 IRI