104
Ona Mkombozi Afa
Kwa unyenyekevu
1. Ona Mkombozi afa,
Deni la haki kulipa.
Afa dhabihu ya dhambi,
Afa dhabihu ya dhambi,
Ili tupate ushindi.
2. Mateso yake wabeza,
Hata mbavu wamchoma;
Kwa dharau na kebehi,
Kwa dharau na kebehi,
Miiba avikwa taji.
3. Akapatwa na mateso
Hakunung’unika neno.
Wajibu atekeleza,
Wajibu atekeleza,
Na Baba amtukuza.
4. “Baba, ondoa kikombe,
Upendavyo, ndivyo iwe.
Nimefanya kazi yako,
Nimefanya kazi yako;
Ipokee yangu Roho.”
5. Alikufa; kwa uchungu,
Jua likaficha nuru!
Na kwa huzuni, dunia,
Na kwa huzuni, dunia
Ikajibu, “Mungu afa!”
6. Aishi— aishi sasa,
Mbele ya hizi ishara,
Twaja kwa unyenyekevu,
Twaja kwa unyenyekevu,
Amri zake kuheshimu.
Maandishi: Eliza R. Snow, 1804–1887
Muziki: George Careless, 1839–1932