84
Imba Twaondoka
Kwa unyenyekevu
1. Imba twaondoka
Tu kimsifu,
Baba wa mbinguni,
Na nyimbo zetu.
Kwa upendo wake,
Kwa kutulinda,
Wimbo wa Sabato
Tutauimba.
2. Msifu kwa wema,
Na kwa rehema.
Kwa baraka zote
Msifu Bwana.
Sauti za shangwe
Ziimbe sana.
Yesu astahili
Shairi bora.
3. Yesu, Mkombozi,
Sasa sikia.
Tunyenyekeapo,
Tunakuomba.
Bwana tuokoe,
Tupe riziki.
Tukutumikie
Kwa usahihi.
Maandishi: George Manwaring, 1854–1889
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906
Zaburi 147:1