56 Bwana Wetu, Upendo Wake Wang’ara Kwa unyenyekevu 1. Bwana wetu, Upendo wake wang’ara Kama nuru na miale yake. Hushawishi, Turudi tena kwa Baba, Kushiriki Utukufu wake. 2. Roho mwema, Hunong’oneza moyoni Yale mema, Kumzidi pepo. Isikike Sauti ya tumaini, Itufunge Kwake kwa upendo. 3. Baba, Mungu, Sikia yetu maombi, Ni ajabu Dhabihu ya Mwana. Asifiwe. Amri zako tutatii. Ee Mfalme, Twakufurahia. Maandishi: Edward L. Hart, 1916–2008. © 1977 IRI Muziki: Crawford Gates, 1921–2018. © 1977 IRI Yohana 15:12–14 Mafundisho na Maagano 34:1–4