170 Wazee wa Israeli Wanaume Kwa ujasiri 1. Wazee wa Israeli twendeni Popote tuwasake wenye haki, Penye jangwa, bahari na misitu, Tuwalete Sayuni wawe huru. [Chorus] O! Babiloni, Babiloni twakuaga; Milima ya Efraemu twaenda. 2. Mavuno mengi wavunaji haba; Tukiungana yote twayaweza. Tutenganishe nganona magugu Toka kifungoni wawekwe huru. [Chorus] O! Babiloni, Babiloni twakuaga; Milima ya Efraemu twaenda. 3. Tuwatembelee nao maskini Wenye njaa na wale wenye dhiki; Tuwafariji kwa injili yake Tuwaonyeshe njia ya milele. [Chorus] O! Babiloni, Babiloni twakuaga; Milima ya Efraemu twaenda. Maandishi: Cyrus H. Wheelock, 1813–1894 Muziki: Thomas H. Bayly, 1797–1839, umefanyiwa marekebisho Mafundisho na Maagano 133:7–9, 14 Mafundisho na Maagano 75:2–5