31
Msifu Aliye Juu
Kwa furaha
1. Msifu aliye juu,
Bwana Mungu Muumba,
Mwamba wa wokovu wetu,
Chanzo cha mamlaka.
Huniponya kwa upendo
Na kuituliza roho.
Sifa kwake milele!
2. Ayafanyayo kwa nguvu
Rehema yahifadhi.
Asubuhi na usiku
Jichowe halilali.
Katika ufalme wake,
Haki hutawala kote!
Sifa kwake milele!
3. Bwana yu karibu nasi,
Kwenye zote taabu,
Daima ndiye auni,
Amani na shauku.
Kama upendo wa mama,
Aongoza wake wana.
Sifa kwake milele!
4. Hivyo, katika taabu
Naimba sifa zako,
Ili wasikie watu
Nakuimbia wimbo.
Moyo, furahia Bwana,
Nawe nafsi, mwili pia!
Sifa kwake milele!
Maandishi: Johann J. Schütz, 1640–1690; yalitafsiriwa na Frances Elizabeth Cox, 1812–1897
Muziki: Kutoka Bohemian Brethren’s Songbook, 1566, umebadilishwa.
Zaburi 104:33
Zaburi 121:2–4