126 Wapendwa wa Mchungaji Kwa utulivu 1. Wapendwa wa Mchungaji, Ni kondoo wapendwa; Tunu pendo awapalo, Tunu kuliko fedha. Wapendwa wa Mchungaji, Na kondoo “wengine”; Milimani awasaka, Hata kina chochote. [Chorus] Jangwani watangatanga, Wasumbuka wapweke; Aenda kuwakomboa, Zizini warudishwe. 2. Wapendwa wa Mchungaji, Ndio wanakondoo; Kuna wanaopotea, Wadhoofika huko. Ona, Mchungaji Mwema, Asaka wapotevu, Awarudisha kwa shangwe, Na kwa gharama kuu. [Chorus] Jangwani watangatanga, Wasumbuka wapweke; Aenda kuwakomboa, Zizini warudishwe. 3. Wapendwa wa Mchungaji, Ni “tisini na tisa.” Apenda wapoteao, Tumaini wakosa. Sikia! Wito wa moyo, Kwa upole asihi: “Hutafuti mpotevu, Aliye mbali nami.” [Chorus] Jangwani watangatanga, Wasumbuka wapweke; Aenda kuwakomboa, Zizini warudishwe. 4. Malisho yanavutia; Maji yenye uhai. Bwana, kwa ari twajibu, “Ndiyo, tunakubali! Tufanye wachunga wako; Tupe pendo la kina. Tutume mbali jangwani, Kondoo kuwasaka.” [Chorus] Jangwani watangatanga, Wasumbuka wapweke; Twendeni kuwakomboa, Zizini warudishwe. Maandishi: Mary B. Wingate, 1845–1933 Muziki: William J. Kirkpatrick, 1838–1921 Luka 15:4–7 1 Petro 5:2–4