61
Ushawishi Moyo Wangu
Kwa hamasa
1. Ushawishi moyo wangu
Nipate imani;
Niyaache ya dunia,
Nipate amani.
2. Nibariki naposali
Moyo uwe mwema,
Nitii sauti ndogo,
Niwe nawe, Bwana.
3. Uniweke patulivu
Na kuniongoza,
Kuzijua njia zako,
Roho kumpata.
4. Bwana, nipe pendo lako
Nisiwe na dhiki.
Ushawishi moyo wangu
Nipate amani.
Maandishi na Muziki: Lorin F. Wheelwright, 1909–1987
© 1958, 1985 Lorin F. Wheelwright. Wimbo huu wa dini ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.