158
Fimbo Ya Chuma
Kwa shangwe
1. Kwa Nefi, mwonaji yule,
Mungu kafunua,
Mfano wa neno lake
Ni fimbo ya chuma.
[Chorus]
Ishike fimbo ya chuma;
Aminifu kweli.
Hii fimbo— neno la Bwana—
Mwongozo thabiti.
2. Tupo bado safarini,
Kwenye majaribu;
Tutapitia gizani,
Penye hatari tu.
[Chorus]
Ishike fimbo ya chuma;
Aminifu kweli.
Hii fimbo— neno la Bwana—
Mwongozo thabiti.
3. Adui akisogea,
Kutisha njiani,
Tushike fimbo ya chuma,
Tuombe auni.
[Chorus]
Ishike fimbo ya chuma;
Aminifu kweli.
Hii fimbo— neno la Bwana—
Mwongozo thabiti.
4. Hatua na kwa hatua,
Siku hadi siku,
Kwa sala na wimbo pia,
Tusonge mbele tu.
[Chorus]
Ishike fimbo ya chuma;
Aminifu kweli.
Hii fimbo— neno la Bwana—
Mwongozo thabiti.
5. Pumziko li karibu,
Yaongoza fimbo,
Tutapata utukufu
Tukishika neno.
[Chorus]
Ishike fimbo ya chuma;
Aminifu kweli.
Hii fimbo— neno la Bwana—
Mwongozo thabiti.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: William Clayson, 1840–1887