75 Mwache Roho Alinde Kwa upole 1. Mwache Roho alinde, Atufunze ukweli, Ashuhudie Kristo, Aonyeshe mbinguni. 2. Mwache Roho aonye, Aongoze chaguzi, Atufikishe pema, Sauti tukitii. 3. Mwache Roho aponye Kwa mamlaka yake, Na tujiweke safi Ili tumpokee. Maandishi: Penelope Moody Allen, kuz. 1939. © 1985 IRI Muziki: Martin Shaw, 1875–1958. © 1915 na J. Curwen & Sons, Ltd. Moroni 10:5–7 Mafundisho na Maagano 11:12–14