114 Njooni kwa Shangwe Kwa sifa 1. Njooni kwa shangwe, Nyote mwaminio! Njooni, mji mwema Bethlehemu. O! Tazameni, Bwana kazaliwa; [Chorus] Njooni tumwabudu; Njooni tumwabudu; Njooni tumwabudu, Kristo, Bwana. 2. Imbeni kwa shangwe, Enyi malaika; Nyote mkaao juu mbinguni! Sifa kwa Mungu, Utukufu kwake! [Chorus] Njooni tumwabudu; Njooni tumwabudu; Njooni tumwabudu, Kristo, Bwana. 3. Tunakusalimu, Asubuhi njema; Na utukufu wote uwe kwako. Mwana wa Baba, Sasa kazaliwa; [Chorus] Njooni tumwabudu; Njooni tumwabudu; Njooni tumwabudu, Kristo, Bwana. Maandishi: Yamehusishwa na John F. Wade, mnamo mwaka 1711–1786; Yametafsiriwa na Frederick Oakeley, 1802–1880 Muziki: Umehusishwa na John F. Wade Luka 2:8–20 Zaburi 95:6