196
Nitachunguza
Kwa hisia
1. Ninayapenda maandiko,
Na ninaposoma,
Namhisi Roho anikuza moyo,
Ukweli kushuhudia.
[Chorus]
Nitachunguza,
Sali na tafakari.
Nitajifunza na kutambua
Maneno ni ya kweli.
2. Nitayasoma maandiko
Mwangu maishani,
Nitazielewa sheria za Bwana.
Atakavyo nitaishi.
[Chorus]
Nitachunguza,
Sali na tafakari.
Nitajifunza na kutambua
Maneno ni ya kweli.
Maandishi: Jaclyn Thomas Milne, kuz. 1949. © 1986 IRI
Muziki: Carol Baker Black, kuz. 1951. © 1986 IRI