190
Nitamuiga Mwokozi
Kwa ujasiri
1. Nitamuiga Mwokozi
Na nitamfuata.
Nitapenda kama yeye,
Kwa ninayoyafanya.
Sichagui vyema kila wakati;
Najitahidi kuisikiliza sauti:
[Chorus]
“Pendaneni apendavyo Yesu.
Mwonyeshe huruma kila mtu.
Onyesha upole na uungwana;
Hivyo Yesu afundisha.”
2. Nitampenda jirani,
Nitamhudumia;
Nasubiri ile siku
Yesu ajapo tena.
Nikijikumbusha mafunzo yake,
Roho atanifundisha tena neno lake:
[Chorus]
“Pendaneni apendavyo Yesu.
Mwonyeshe huruma kila mtu.
Onyesha upole na uungwana;
Hivyo Yesu afundisha.”
Maandishi na muziki: Janice Kapp Perry, kuz. 1938
© 1980 na Janice Kapp Perry. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.