76 Sala ya Faragha Kwa kutafakari 1. Kuna muda mtulivu, Pasipo karaha; Mbele ya Bwana nasali Sala ya faragha. [Chorus] Moyo na ugeuke, Kuomba siku zote, Na ili nafsi yangu Iungane na mbingu. 2. Njia nyofu ya mbinguni, Wapo malaika, Twaipata tufanyapo, Sala ya faragha. [Chorus] Moyo na ugeuke, Kuomba siku zote, Na ili nafsi yangu Iungane na mbingu. 3. Dhoruba nipitiapo, Ni faraja kwamba, Bwana husikia ile, Sala ya faragha. [Chorus] Moyo na ugeuke, Kuomba siku zote, Na ili nafsi yangu Iungane na mbingu. 4. Adui anitegapo, Mwokozi namwita, Huja kama nitasali, Sala ya faragha. [Chorus] Moyo na ugeuke, Kuomba siku zote, Na ili nafsi yangu Iungane na mbingu. Maandishi na muziki: Hans Henry Petersen, 1835–1909 Mathayo 6:6 Alma 33:3–11