103
Mungu Kamtuma Kwetu
Kwa heshima
1. Mungu kamtuma kwetu—
Mpatanishaji Yesu—
Kutuelekeza njia
Ya kurudi kwake Baba.
2. Na akawa mwanadamu,
Akakubali adhabu.
Akafa bila hatia,
Kuifidia sheria.
3. Upendo mtakatifu!
Nastahili kushukuru,
Kwamba kwa thabihu yake
Nakaa moyoni mwake.
4. Kwa mwenendo anataka
Nijiweke kama mwana,
Ninyenyekee nifunzwe
Na Mtakatifu pekee.
5. Sakramenti twashiriki
Dhabihu twatafakari,
Kwamba neno twatimiza
Na kumkumbuka Bwana.
Maandishi: Edward P. Kimball, 1882–1937
Muziki: Alexander Schreiner, 1901–1987. © 1948 IRI