49
Niongoze
Kwa hamasa
1. Yesu, Mkombozi,
Niongoze.
Nakata shauri,
Niongoze.
Hata kwenye giza,
Na kunapokucha.
Uwe wangu mwanga.
Niongoze.
2. Hata kwenye shida,
Niongoze.
Nifundishe wema.
Niongoze.
Nguvu ya wokovu
Iwe kila siku,
Bwana, kinga yangu.
Niongoze.
3. Niwapo na dhambi,
Niongoze.
Nikiwa na jonzi,
Niongoze.
Inapotoweka
Amani na raha,
Nijaze neema,
Niongoze.
4. Kikifika kifo,
Niongoze.
Nitulize moyo.
Niongoze.
Unihurumie
Ili upendowe
Kwako unilete.
Niongoze.
Maandishi na muziki: Orson Pratt Huish, 1851–1932