176 Familia Huwa za Milele Kwa uchangamfu 1. Nina familia yangu. Na kwangu ni wema. Nataka niishi nao milele daima. [Chorus] Familia huwa za milele Kwa mpango wa Baba. Niwe na familia yangu daima Na Bwana amenionesha, Amenionesha njia. 2. Nikiwa bado mdogo, Vyema nijiandae, Nikafunge hekaluni ndoa ya milele. [Chorus] Familia huwa za milele Kwa mpango wa Baba. Niwe na familia yangu daima Na Bwana amenionesha, Amenionesha njia. Maandishi: Ruth M. Gardner, 1927–1999. © 1980 IRI Muziki: Vanja Y. Watkins, kuz. 1938. © 1980 IRI Mafundisho na Maagano 138:47–48 Alma 37:35