11 Asante Mungu kwa Nabii Kwa uchangamfu 1. Asante Mungu kwa nabii, Kutuongoza hizi siku. Asante kuleta injili, Iongezayo ufahamu. Asante kwa kila baraka, Pia kwa ukarimu wako. Twapenda kukutumikia Na kuzitii amri zako. 2. Na shida zinapotuzonga, Na kutisha amani yetu, Matumaini hutujia, Kwamba wokovu u karibu. Hatuna mashaka kwa Mungu Ni dhahiri toka zamani. Hakika wataangamizwa Waovu wapinga Sayuni. 3. Tutamsifu siku zote. Rehema zake tutaimba, Tufurahie injiliye, Na mwangaza wenye uzima. Ukamilifu wa milele Watapewa waaminifu, Wakanao injili hii Furaha hawata fahamu. Maandishi: William Fowler, 1830–1865 Muziki: Caroline Sheridan Norton, 1808–mnamo 1877 Mafundisho na Maagano 21:1–5 Mosia 2:41