156
Ukweli Ni Nini?
Kwa ujasiri
1. Ukweli ni nini? Thamaniye
Huzidi vito na dhahabu,
Na ubora utaonekana pale
Ambapo utajiri wote wa falme
Utaonwa kama uchafu.
2. Ukweli ni nini? Tuzo zuri
Watu na mbingu kuwania.
Utafute ung’aripo kilindini,
Au ufukuzie hadi mbinguni:
Ni lengo la kutamaniwa.
3. Mwonevu nguvu atazidiwa
Ataposhindana na haki.
Hivyo ukweli utadumu daima,
Na ngome yake kuhimili vimbunga
Na mapinduzi ya katili.
4. Hivyo, ukweli ni mwisho na mwanzo,
Msimu, nyakati hauna.
Japo mbingu, nchi zitafika mwisho,
Ukweli, uhalisi, utakuwepo,
Kubakia hivyo, daima.
Maandishi: John Jaques, 1827–1900
Muziki: Ellen Knowles Melling, 1820–1905
Mafundisho na Maagano 93:23–28
Yohana 18:37–38