Muziki
Ee Mwokozi, Mkombozi


50

Ee Mwokozi, Mkombozi

Kwa unyenyekevu

1. Ee Mwokozi, Mkombozi,

Tupe ujumbe wako.

Naye Roho wako aje,

Atujaze mioyo;

Tusadiki neno lako

Tutoke kwenye dhambi.

Ee Mwokozi, Mkombozi,

Zikae kwako nafsi.

2. Ee Mwokozi, Mkombozi,

Tazama, tu wanyonge,

Katika upendo wako,

Dhambi tuepushie.

Tuzingire kwa upendo,

Tuweke kwenye njia.

Ee Mwokozi, Mkombozi,

Tuwe nawe daima.

3. Ee Mwokozi, Mkombozi,

Mioyo ifariji,

Tusije tukafa moyo,

Tupanguze machozi.

Tuepushe na dhoruba,

Bahari itulize,

Ee Mwokozi, Mkombozi,

Amani yako tupe.

Maandishi na muziki: H. R. Palmer, 1834–1907

Isaya 26:3–4

Zaburi 145:8–9, 14–21