55 Mwokozi wa Nafsi Yangu Kwa unyenyekevu 1. Mwokozi wa nafsi yangu, Mkono wako na nguvu Umenifanya mzima, Majonzi yakawa raha! Sinayo lugha kinywani, Kukusifu Mkombozi. 2. Sitoweza kukulipa, Lakini nitakupenda. Neno lako takatifu, Si ndilo furaha yangu? Liwe yangu simulizi, Tena nikutafakari. 3. Nitende yako mapenzi. Adui awe rafiki, Na nafsi nirekebishe Hadi niwiane nawe. Nistahilishe upendo, Nifae maisha yako. Maandishi: Orson F. Whitney, 1855–1931 Muziki: Harry A. Dean, 1892–1987. © 1948 IRI 2 Nefi 1:15 Mafundisho na Maagano 95:1