148 Tunasimama Sayuni Kwa uthabiti 1. Tunasimama Sayuni Vijana shupavu, Ahadi yatung’aria, Wajibu ni wetu, Msingi wa maadili Kuuendeleza. Twazimudu changamoto— Wakweli daima! 2. Ukweli tufuatao Wadharaulika. Lakini tunapotii Twajua twaweza Kuyahimili maovu Yaangamizayo. Tunayo fimbo ya chuma, Furaha ilimo. 3. Hofu na jaribu huja, Ila hatuhofu. Ni kwa ajili ya haki Tunauthubutu. Tutapenda, tutashinda; Wimbo tutaimba Kama vijana Sayuni— Wasafi, imara. Maandishi: Susan Evans McCloud, kuz. 1945. © 1985 IRI Muziki: Lahani ya Ayalandi; mpangilio © 1985 IRI Alma 37:35–37 Alma 53:20–21