115
Kwenye Mji wa Daudi
Kwa utulivu
1. Kwenye mji wa Daudi
Kwenye zizi la ng’ombe,
Ndipo mama kamlaza
Horini mwana wake;
Mama mpole Maria,
Yesu mwanae mchanga.
2. Alikuja duniani,
Bwana Mungu wa wote.
Kwenye nyasi alilala,
Zizi hifadhi yake;
Wapole nao maskini,
Kristo aliwathamini.
3. Na sote tutamuona
Kwa wake ukombozi,
Kwani mtoto mpole
Ni Mungu wa mbinguni;
Huwaongoza watoto
Mahali ambapo yupo.
Maneno: Cecil Frances Alexander, 1818–1895
Muziki: Henry J. Gauntlett, 1805–1876