195 Nitamtafuta Ujanani Kwa hamasa Nitamtafuta ujanani, Bwana anifunze ukweli. Nitalisoma neno lake, Kisha Mungu Baba nimuombe. Nitamtafuta na kutii Maneno yote ya nabii. Nitafuata amri zake zote. Nitamtafuta Bwana nimpate. Maandishi na Muziki: Joanne Bushman Doxey, kuz. 1932. © 1984 IRI Mafundisho na Maagano 88:63 Isaya 55:6 Zaburi 63:1