173 Vyote Vyenye Uzuri Kwa shukurani 1. Kwa kila ua dogo, Ndege wa kuimba, Kawapa rangi nzuri, Kawapa na mbawa. [Chorus] Vyote vyenye uzuri, Miti na wanyama, Vyote vyenye fahari Bwana kaviumba. 2. Kilele cha mlima, Mto wamwagika, Jua lichomozapo Huangaza anga. [Chorus] Vyote vyenye uzuri, Miti na wanyama, Vyote vyenye fahari Bwana kaviumba. 3. Upepo wa baridi, Kiangazi chema, Matunda bustanini, Kayatengeneza. [Chorus] Vyote vyenye uzuri, Miti na wanyama, Vyote vyenye fahari Bwana kaviumba. 4. Miti yenye kijani, Konde zavutia, Kando kando ya maji Tunakusanyika. [Chorus] Vyote vyenye uzuri, Miti na wanyama, Vyote vyenye fahari Bwana kaviumba. Maandishi: Cecil Frances Alexander, 1818–1895 Muziki: Tuni ya Kingereza ya Kale. Umepangiliwa © 1989 IRI 2 Nefi 2:14 Mwanzo 1:1, 31