99 Tusifu Jina la Bwana Kwa hamasa 1. Tusifu jina la Bwana, Atukuzwe Yesu, Aliyekufa Golgotha, Kutuweka huru. 2. Aliyashinda mauti, Kuleta wokovu, Wenye dhambi kawaita, Kuishi kwa Mungu. 3. Kashinda nguvu za kifo, Kamshinda nyoka, Amefungua kaburi, Wafu kafufua. 4. Sakramenti ni ishara Ya dhambi kuoshwa, Shirikini na kukiri Mnamkumbuka. Maandishi: Richard Alldridge, 1815–1896 Muziki: Joseph Coslett, 1850–1910 2 Nefi 9:5, 10–12 Musa 4:20–21