67 Najua Bwana Aishi Kwa furaha 1. Najua Bwana aishi, Mwokozi, Mwana wa Mungu, Aliyekishinda kifo, Kristo, Mkombozi wangu. 2. Mwamba wangu anaishi, Ndiye tumaini letu, Mwangaza uongozao, Hadi tufikie mbingu. 3. Nipe Roho wako, Bwana, Nipate amani yako. Nipe imani nipite Njia irudiyo kwako. Maandishi: Gordon B. Hinckley, 1910–2008. © 1985 IRI Muziki: G. Homer Durham, 1911–1985. © 1985 IRI Mafundisho na Maagano 76:22–24, 41–42 Ayubu 19:25