145
Weka Zako Juhudi
Kwa shauku
1. Waitwa wenye dhamira
Ya wachapakazi.
Njoo kazi tuifanye;
Weka zako juhudi.
[Chorus]
Weka zako juhudi; kwa hamu.
Fanya kwa moyo wenye uhuru.
Tuna kazi; tusibaki.
Weka zako juhudi
2. Kanisa linatafuta
Watu saidizi.
Kazi za kufanya zipo;
Weka zako juhudi.
[Chorus]
Weka zako juhudi; kwa hamu.
Fanya kwa moyo wenye uhuru.
Tuna kazi; tusibaki.
Weka zako juhudi.
3. Basi usikae bure;
Pambana na dhambi.
Vita ina endelea;
Weka zako juhudi.
[Chorus]
Weka zako juhudi; kwa hamu.
Fanya kwa moyo wenye uhuru.
Tuna kazi; tusibaki.
Weka zako juhudi.
4. Basi omba na pambana
Kwa nguvu na ari.
Fanya kila jambo jema;
Weka zako juhudi.
[Chorus]
Weka zako juhudi; kwa hamu.
Fanya kwa moyo wenye uhuru.
Tuna kazi; tusibaki.
Weka zako juhudi.
Maandishi na muziki: Will L. Thompson, 1847–1909